(+video) Muigizaji asimulia kuchumbiana na wanaume 5 kwa wakati mmoja, kula mahari yao

Pennie ni muigizaji anayeshiriki kipindi muendelezo cha Sinia katika DSTV.

Muhtasari

• Muigizaji huyo alisema alifuatwa na wanaume 5 kwa wakati mmoja kila mmoja akitaka kumuoa.

• Alisema aliitisha kila mmoja mahari ili aende kujilipia kwa wazazi na kuwapoteza kwa kusema kwamba hakuwa na mapenzi nao.

Muigizaji Pennie ambaye alijizolea umaarufu nchini Tanzania na nje kutokana na kushiriki katika muendelezo wa filamu ya Sinia inayopeperushwa kwenye DSTV Jumatano alifunguka makubwa kuhusu maisha yake ya kimapenzi na jinsi alivyochumbiana na wanaume kadhaa na kula mahari yao kabla ya kuwapotezea.

Akizungumza katika kipindi cha Lavi Davi katika kituo cha Wasafi, Pennie alisema kwamba ni kweli aliwahi chumbiana na wanaume hao wote amabo kila mmoja alimfuata kwa wakati wake akitaka kuuoa na yeye aliwaaminisha kwamba yuko tayari kwa ndoa na alipokula mahari yao akawapotezea kwa kile alisema hakuwa na mapenzi nao hata kidogo.

“Walinifuata wanaume watano. Unajua mtu ukishampenda unamwaminisha kila kitu hata akuambieje, na kwa upande wetu sisi wasichana mwanaume akikupenda anakuwa dhaifu. Mimi niliwaaminisha japokuwa sikuwa na mapenzi. Wa kwanza nilimuaminisha akanipa pesa nipeleke kwetu kama mahari na mwisho wa siku niyatia kibindoni na hakuna ambalo hangenifanya,” alisema Pennie.

Alisema kwamba hakuwa kabisa na dhamira ya kupenda ila tu tamaa ya pesa na kusema kwa vile alikuwa anajua siku hizi wasichana wengi wanaumizwa katika mapenzi na wavulana wasiotulia, usiku na mchana wanadanga utadhani kina dada wa baleghe.

Alisema kwamba hajutii kuwafanyia wanaume kitendo hicho kwani siku hizi wanaume wengi hawapendi kuwajibika katika mahusiano bali wanapenda tu kushusha kitonga kwa wanawake wanaoona wana afadhali katika upande wa riziki.

Matukio ya Wasichana Kuumizwa Kwenye Mahusiano Yamekuwa mengi Sana...Unaweza kujiona uko peke yako kumbe Mpo wengi..Tunaishi Kwa Akili. Wavulana wengi Siku hizi Wamekuwa wavivu hawapendi kujituma....Wanataka Sisi Wasichana Ndio tuwalee na tufanye Kila kitu Kwenye Mahusiano Wabadilike,” alisema Pennie kwa ukakamavu mkubwa.