Guardian Angel arusha shoo ya moto Kasarani kuapishwa kwa Ruto

Mshereheshaji Chipukeezy aliwatambulisha wasanii hao katika uwanja wa Kasarani.

Muhtasari

• Vikosi mbali mbali vya wasanii vilijitoma kati kati ya uwanja huo punde baada ya Ruto kuapishwa na idara ya majeshi kuviondoa vikosi uwanjani.

Mwanamuziki Guardian Angel atumbuiza shoo ya moto
Mwanamuziki Guardian Angel atumbuiza shoo ya moto
Image: Instagram

Mwenyekiti wa wasanii wa injili Kenya Guardian Angel alikuwa miongoni mwa wasanii waliochaguliwa kutumbuiza katika ukumbi wa Kasarani wakati rais wa tano William Ruto alikuwa anaapishwa.

Vikosi mbali mbali vya wasanii vilijitoma kati kati ya uwanja huo punde baada ya Ruto kuapishwa na idara ya majeshi kuviondoa vikosi uwanjani.

Guardian Angel alikuwa wa pili kutumbuiza ambapo alitumbuiza kwa kibao chake cha Kenya amabcho kina maudhui ya kuwataka Wakenya kuungana pamoja na kushikana mikono kuijenga nchi.

“Wananchi wote tushikane mikono tuijenge Kenya, tusiwatukane viongozi mitandaoni, kina mama jifungeni maleso,” baadhi ya mistari kwenye wimbo huo inaimba.

Wimbo huu ndio ulioonekana kuwagusa watu wengi katika uwanja huo ambapo rais Ruto alionekana akichezesha kichwa kuendana na midundo ya wimbo huo.

Angel akiwa na wacheza densi mahiri, walinogesha kibao hicho ambacho baada ya kumaliza kucheza wakenya wengi katika mitandao ya kijamii walimmiminia sifa kwa kusema kwamba alifanya kazi nzuri na inaonesha ni kwa nini alistahiki ile nafasi muhali kutokea kwa wasanii nchini.

“Kwa kweli Guardian Angel ile nayo ilikuwa moto, yaani mpaka kila mtu akashangilia,” mmoja aliandika