Hatimaye Harmonize amkutanisha bintiye wa damu, Zuhu Konde na binti wa kambo, Paula

Harmonize alitembelea duka la Paula la kuuza nguo akiwa na bintiye Zuhu na kuwakutanisha.

Muhtasari

•  Paula alionekana kweney video akiwa amembeba dadake kutoka kwa mama mwingine huku akionesha tabasamu na furaha. 

Harmonize amkutanisha Paula na bintiye
Harmonize amkutanisha Paula na bintiye
Image: Instagram screengrab

Familia ya msanii Harmonzie kutoka Konde Gang inazidi kufuatiliwa sana kwenye mitandao ya kijamii kama moja ya familia pendwa kwa mwaka huu.

Baada ya muda mrefu wa watu kuzua mitandaoni kuwa msanii huyo hatoweza kupikika kwenye chungu kimoja na Paula Kajala ambaye nib inti wa mchumba wake, Kajala Masanja, hatimaye familia hiyo imekiuka hili na kuwatupia kovu la kudumu wambea wafitinishaji.

Harmonize Alhamis alitembelea duka la kuuza nguo la Paula Kajala ambapo pia aliandamana na bintiye wa kumzaa kwa jina Zuhu Konde kwenda kwenye duka hilo la nguo.

Harmonize alifanya kitendo hicho mahususi ili kumkutanisha bintiye wa damu na Paula ambaye sasa hivi amemkubali kama baba wa kambo haswa baada ya kumvisha mamake pete ya uchumba.

Katika video ambazo Harmonize alipakia kwenye Instastories zake, anaonekana akimchagulia nguo kadhaa bintiye Zuhu huku binti huyo akiwa ameshikilia jezi ya timu ya Yanga. Harmonize anamuuliza bintiye kama yeye ni shabiki wa Yanga, jambo ambalo binti huyo anakubali kwa kutikiza kichwa na msanii huyo kuruka juu kwa furaha kwa kile anasema kuwa huo ndio urithi kamili anaomrithisha kwani pia yeye ni shabiki kindakindaki wa Yanga SC.

Kwenye klipu nyingine, Paula anaonekana amembeba Zuhu ambaye sasa ni dadake mwingine mikononi huku akitabasamu kwa furaha kukutanishwa na dadake kutoka kwa mama mwingine.

Wengi wamesubiri sana kama kutakuwepo na harusi ambayo Harmonize na Kajala wamekuwa wakiidokeza kwa miezi kadhaa sasa.

Itakumbukwa kwamba juzi familia hiyo kwa maana ya Harmonize, Kajala na Paula walielekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuchukua mzigo wa nguo ambazo juzi zimetua katika duka la Paula la nguo. Duka hilo ambalo Mwijaku alisema ni Harmonize aliweza kumfungulia Paula kama njia moja ya kufuta mikwaruzano ya nyuma.