Mwijaku asema Kajala anamuuza bintiye Paula kwa Harmonize sababu ya njaa

Mtangazaji huyo alizidi kusema kuwa watatu hao wanashiriki kulala katika kitanda kimoja

Muhtasari

• Mwijaku alizidi kusema kuwa Kajala alimuuza kimapenzi bintiye kwa Harmonize baada ya kupewa gari aina ya Range

Mwijaku aibuka na jipya kuhusu Mahusiano ya Kajala bintiye Paula na Harmonize
Mwijaku aibuka na jipya kuhusu Mahusiano ya Kajala bintiye Paula na Harmonize
Image: Instagram

Hivi karibuni Harmonize aliweka wazi kuwa hataki kuwa na chawa yeyote ili kudumu katika muziki wa Bongo Fleva amabo wasanii wengi wana machawa kwa maana ya watu wanaowatetea kinafiki kwa hali na mali.

Kila mtu alikuwa anajua msanii huyo alikuwa anamlenga mtangazaji Mwijaku ambaye tangu kuondoka Wasafi amekuwa akionekana kumtetea huku akimkandia Diamond.

Mwijaku naye hayakimya kwani ndio mwanzo ameendeleza sekeseke zake za kumshambulia Harmonize vikali.

Jumanne baada ya Harmonize kupakia video fulani kwenye instastories zake akionekana kuwa katika duka la jumla moja nchini Afrika Kusini ambapo walikuwa na mchumba wake Kajala, binti yao Paula pia alipakia picha ikimuonesha ako katika sehemu hiyo hiyo moja Afrika Kusini.

Hili lilizua mjadala mkali mitandaoni haswa baada ya Mwijaku kuandika kwenye Tweeter yake akimrushia dongo Harmonize kwa kusema kuwa anawatumia Kajala na binti yake wote kimapenzi.

Mwijaku alimzomea vikali Kajala Masanja kwa kusema kuwa alipewa gari aina ya Range pamoja na vitu vingine alivyovitaja kama vya kumrubuni ili kukubali kutumiwa kimapenzi na Harmonize ambaye pia Mwijaku alisema anamtumia hata binti yake, Paula.

Mwijaku alizidi kuvuka mipaka ya heshima kwa kusema kuwa hata watatu hao, Harmoni, Kajala na binti yake Paula wanashiriki kitendo katika kitanda kimoja na kusema kuwa Kajala na binti yake wanafanya hivyo kutokana na njaa.

“Mama anamuuza mtoto kisa Range na kodi ya pango la duka. Naumia sana kuona mama anamdangisha mtoto wake kwa mwanaume ambaye na yeye anatembea naye kisa kodi ya pango na gari la kutembelea. Wazazi malezi yako wapi? Mtoto anashiriki kitanda kimoja na mzazi kushiriki mapenzi. Kweli njaa mbaya sana,” Mwijaku aliandika.