Baadhi ya wazazi wapya maarufu ambao hawakupigia debe ujauzito wao

Baadhi ya watu maarufu walipitia safari ya ujauzito bila kutangaza kuhusu maendeleo ya kipindi hicho.

Muhtasari

• Wengine hawakuangazia suala hilo kama lengo kuu la kuwatumbuiza mashabiki wao kwa sababu zao kama kutokuwa na haja ya kutafuta kiki wala kuwatumbuiza mahabiki wao.

Zia Bett na Celestine Ndinda

Baadhi ya Wakenya wamejitwika jukumu la kuwa wazazi mwaka huu, wengine wakiwa wamejifungua huku wengine bado wakiwa katika safari ya ujauzito. 

Baadhi ya watu maarufu walipitia safari ya ujauzito hadi kujifungua bila kuwatangazia mashabiki wao kuhusu maendeleo ya kipindi hicho

Baadhi ya watu maarufu ambao wamekuwa katika safari ya ujauzito ila hawakueneza hali yao ni:

Nameless na Wahu Kagwi

Nameless na Wahu walitangaza kuwa wanatarajia mtoto wa tatu ila hawakuzungumzia sana maendeleo ya ujauzito mitandaoni.

Wahu alijifungua wiki iliyopita Jumanne ambapo alitangaza habari hizo njema na hata kufichua sura ya mtoto wao.

Njugush na Celestine Ndinda

Wanandoa hao hawakuwa wamewajulisha wanamitandao wala mashabiki wao kuhusu uja uzito wao kwa muda. Haikuwahi julikana mtandaoni kuwa Ndinda alikuwa mja mzito hadi walipotangaza wenyewe.

Wawili hawa walitangaza uja uzito huo kupitia hafla waliokuwa wameandaa ya kutazama filamu iliyohudhuriwa na watu wengi. Hata hivyo, mkewe Njugush, Celestine alijifungua hivi majuzi na kuwajulisha mashabiki wao baada ya mwezi mmoja wa kujifungua.

Julani na Lilian Ng'ang'a

Mwanamuziki Juliani na mkewe Ng'anga Lilian walimpokea mwanao miezi miwili na ushee iliyopita.

Wawili hao walikuwa wamejaribu sana kuuficha uja uzito huo lakini wanamitandao walijua.

Pascal Tokodi na Grace Ekirapa

Wanandoa hao walimkaribisha binti yao ulimwenguni mwezi wa Aprili. Wawili hao hawakuchukulia suala hilo kama jambo la kuwatumbuiza mashabiki wao wala kupiga debe.

Nyashinski na mke wake Zia Bett

Mwanamuziki Nyashinski na mke wake Zia Bett hawakutangaza ujauzito wao ila Zia alijulikana kuwa mjamzito baada ya kupakia picha yake kwenye Instagram katika tangazo la nguo bora za kuvalia wakati wa ujauzito. 

Wapenzi hao hawajaongelea kuhusu ujauzito huo wala kutaka kuwaonyesha mashabiki wao safari ya uja uzito huo.