(+video) Baraka mfululizo! Nameless na Wahu wabarikiwa na mtoto wa tatu

Walikuwa wamechumbiana kwa miaka minane kabla ya kufunga ndoa mwaka wa 2005.

Muhtasari

• Waliwashukuru wote kwa ushirikiano wao na kuwatakia mema kwenye safari hiyo ya uja uzito ambayo imekamilika leo.

Wahu// Nameless

Wanamuziki Nameless na Wahu wametangaza kuwa wamemkaribisha binti yao wa tatu leo siku chache baada ya sherehe ya uja uzito wake.

Wawili hao wametangaza jina la mtoto wao waliyemwita Shiru.

"Hii ni baada ya dakika tano alipozaliwa .Huu ni muunganisho wa kwanza duniani na binti yangu wa tatu, Shiru, ambaye tumpempa jina la dada yangu mkubwa Rosemary kulingana na mila ya Kikuyu," Nameless alisema.

Waliwashukuru wote kwa ushirikiano wao na kuwatakia mema kwenye safari hiyo ya uja uzito ambayo imekamilika leo.

"Asanteni sana  kwa maombi yenu. Shiru ana afya njema,mrembo na mke wangu, mama Shiru alifanya kazi murwa kwa kumleta duniani binti yetu," Nameless alisema kwenye chapisho la Instagram.

Alifichua kuwa alikuwa kwenye chumba cha kujifungua wakati mkewe alikuwa anajifungua na alisema kuwa Wahu yu buheri wa afya na kuwa wako tayari kumlea binti yao pamoja .

Nameless alionekana kuwa mwenye furaha huku akimbeba bintiye na kumbusu.

Nameless anajiita mwenyekiti wa chama cha baba mabinti na kundi la kulea watoto wa kike, na ameonesha imani yake kubwa kwa binti yake kifungua mimba kwa jina Tumiso na kusema kuwa amejiweka tayari kabisa kuwaongoza dada zake wadogo.

Wanamuziki hao pia walifichua sura ya binti wao hata baada ya wanamitandao kutarajia kuwa watafichua sura ya binti yao katika muda mchache wa kuzaliwa.

Nameless na Wahu wamemkaribisha binti yao baada ya kuwa kwenye ndoa kwa miaka 17 na kubarikiwa na mabinti wa kwanza wawili.

Walikuwa wamechumbiana kwa miaka minane kabla ya kufunga ndoa mwaka wa 2005.