(+video) Kizz Daniel amuiga Harmonize, akohoa kwenye wimbo wake mpya

Msanii huyo alipakia kionjo cha wimbo wake ODO ambao unatarajiwa kuachiwa rasmi mwishoni mwa wiki hii.

Muhtasari

• Katika kionjo cha wimbo huo ambacho alikipakia Instagram, Kizz Daniel anasikika akianza kwa kukohoa kama kuiga kibwagizo cha msanii Harmonize.

Msanii Maarufu kutoka Nigeria, Kizz Daniel kwa mara nyingine tena ameachia kionjo cha kibao chake kipya ambacho kinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki hii.

Kama ilivyotarajiwa, kionjo hicho kimepata mapokezi makubwa sana kutoka kwa mashabiki wake baada ya kupakia kipande hicho kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mkali huyo wa kibao cha Buga alifagiliwa nqa wengi baada ya kuibuka na mafanikio makubwa katika safari yake kwenye muziki, safari ambayo haina muda mrefu tangu awekeze muda wake rasmi kweney tasnia ya muziki wa Afrobeats.

Kilichoshangaza wengi haswa mashabiki wa muziki kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, Buga alianza kionjo hicho cha wimbo wake akikohoa, kama kuiga kibwagizo cha msanii Harmonzie ambaye katika ngoma zake huanza aghalabu kwa kukohoa.

Wimbo huo ambao Kizz Daniel alidokeza mpaka jina lake kuwa utaitwa Odo ama Cough alisemwa kuwa ameiga Harmonize katika kukohoa huko ambako kumempa upekee katika kazi zake nyingi haswa mwaka huu.

Wadau wa muziki haswa kutoka nchini Tanzania na ambao ni wakereketwa wa msanii Harmonize walipata kupagawa kishenzi baada ya kusikia kwamba msanii huyo kutoka Nigeria amepata kuiga Harmoniz, ishara ambayo waliisema kuwa huenda msanii huyo kwa muda mrefu amekuwa akiufuatilia muziki wa Harmonize kwa muda na hata kuvutiwa na kibwagizo hicho cha kukohoa.

Wengine walimsifia Harmonize kwa kuibuka na kibwagizo cha kipekee ambacho sasa kimefanya muziki wake kupenya hadi kwenye mataifa ya kigeni na kusikilizwa na watu tajika katika tasnia pana ya muziki.