Diamond akae mbali na nyinyi - Shabiki awaambia Zari na Shakib.

Shabiki huyo alifurahishwa na mahaba yaliyoko kati ya Zari na Shakib

Muhtasari

• Shabiki huyo alikuwa anampa ushauri mpenzi wake Shakib, Zari Hassan wa kujitenga na mpenzi wake wa hapo awali, Diamond. 

Zari Hassan na mpenzi wake Shakib Cham.
Image: HISANI

Shabiki mmoja alichukua hatua ya kuwashauri wapenzi maarufu Zari Hassan na Shakib Cham Lutaaya dhidi ya mwanamuziki Diamond.

Shabiki huyo alitoa maoni hayo baada ya Shakib kupakia picha zake na Zari katika ukurasa wake wa Instagram.

Alikuwa miongoni mwa mashabiki wa wapenzi hao wawili kuwaonyesha kuwa wanaunga mkono uhusiano huo.

Aliwaambia wapenzi hao kuwa mpenzi huyo wa hapo awali wa Zari hafai kuhusishwa katika maisha yao wawili.

"Diamond anapaswa kukaa mbali na nyinyi, yeye ni mnafiki tu," Stellagoddy alimwambia Zari.

Shakib alikuwa amepakia picha zilizoonyesha mahaba yaliyoko baina yake na mpenzi wake Zari.

Katika picha hizo, wapenzi hao wawili walikuwa wakifurahia maankuli yao walipokuwa kwenye mtoko wa hivi majuzi.

Alitoa maoni yaliyoonyesha upendo wake kwa mwanasosholaiti huyo na jinsi alivyofurahi kuwa kwenye uhusiano naye.

"Mioyo miwili iligeuka ikawa  moja," Cham aliandika huku akiashiria mapenzi yake na Zari.

Zari pia hakusita kukubaliana na maoni hayo ya mpenzi wake na aliandika huku pia yeye akimwonyesha mahaba.

"King K," mama huyo wa watoto watano alisema.

Hivi majuzi, ilifichuka kuwa Zari na Shakib wamekuwa katika mahusiano yao kwa miaka minne baada ya Zari kuachana na mwanamuziki Diamond.

Shaki alifichua haya katika ukurasa wake wa TikTok baada ya kupakia video iliyoonyesha kumbukumba zao wakiwa pamaoja.

Zaidi ya hayo, mwanasosholaiti huyo alidokeza kufung pingu za maisha na mpenzi huyo wake mdogo.

Ailisema kuwa mpenzi huyo wake alikuwa anapanga kupeleka posa kwa wazazi wake Zari nchini Uganda ili amuoe.

Zari alibainisha kuwa mapenzi hayo yake na Bw Shakib Cham yamemletea amani katika maisha yake na yamewezesha kung'aa zaidi.