Wahu amsifia bintiye Tumiso kwa kumsaidia kulea mziwanda Shiru

Wahu alipendezwa na jinsi Tumiso alivyowajibika kumlea dada yake mdogo

Muhtasari

Mwanamuziki huyo alionyesha ukaribu ulioko baina ya mabinti wake wawili na jinsi Tumiso anavyomsaidia kulea kitinda mimba wao.

Tumiso na Shiru

Mwanamuziki Wahu ameonyesha jinsi binti yake wa kwanza alivyopenda jukumu lake la kuwa kifungua mimba.

Katika picha aliyopakia Instagram, Tumiso alionekana akimbeba dada yake mdogo, Shiru huku akimbusu.

Wahu alionyesha kufurahishwa na ukaribu wa Tumiso na Shiru kwa jinsi binti yake alivyokuwa anamwonyesha dada yake upendo.

"Picha moja inayoonyesha hisia nyingi za kupendeza, mapenzi matamu," Wahu aliandika .

Alimpongeza Tumiso kwa kuwa binti anayemsaidia katika malezi ya dada yake mdogo kama mama mlezi.

Kabla ya Wahu kujifungua, Nameless alikuwa amesema jinsi binti yake wa kwanza alikuwa ameonyesha kuwa tayari kuwaongoza dada zake wadogo.

Alisema kuwa Tumiso alikuwa tayari kuwa mfano mwema kwa dada yake Nyakio na kumlea kitindamimba Shiru.

Wahu amezidi kuwaonyesha mabinti wake upendo na kuwapa malezi bora hata watu wanapowahimiza kupata mtoto wa kiume.

Mwanamuziki huyo na mume wake wamepuuzilia mbali shinikizo la watumizi wa mitandao ya kijamii la kuzaa mtoto wa kiume.

Mapema wiki hii, msanii Wahu alimjibu mtumizi mmoja wa mtandao wa Facebook aliyetaka kujua iwapo yeye na mume wake wana dhamira ya kutuma maombi kwa Mungu kwa ajili ya mtoto wa kiume, swali ambalo Wahu alimjibu kwamba ametosheka na baraka ya mabinti watatu aliojaliwa mpaka sasa miaka 25 katika mahusianio.

 

"Sina haja ya kumtafuta mtoto wa kiume hata kidogo... Nina furaha na nimeridhika na mabinti wangu." Staa huyo wa 'Back It Up' alijibu kwa madaha.

Wahu amekuwa akionyesha upendo wake kwa mabinti wake na jinsi alivyoridhika mno kujifungua watoto wa kike mwengine.