Lilian Ng'ang'a arudi katika kazi ya mjengo miezi 3 baada ya kujifungua mtoto

Ng'ang'a alionekana katika eneo la mjengo huku amevalia mawanda ya kazi hiyo.

Muhtasari

• Mama wa mtoto mmoja hivi majuzi alipakia muonekano wake mpya baada ya miezi 3 ya kujifungua.

Ng'ang'a atangaza kurejea kazini baada ya kujifungua
Ng'ang'a atangaza kurejea kazini baada ya kujifungua
Image: Instagram

Aliyekuwa mama kaunti ya Machakos, Lilian Ng’ang’a amerejea katika kazi zake za kawaida kupanga kazi za ujenzi wiki kadhaa baada ya kujifungua mtoto.

Mama wa mtoto mmoja hivi majuzi alipakia umbile lake jipya baada ya miezi 3 ya kujifungua. Lillian alifurahia siku moja ya wikendi na kuchapisha video adimu akiwa yeye tu.

Ng’ang’a alichapisha kupitia Instastories zake kwamba amerejea kazini baada ya miezi kadhaa ya kukaa nje ya umaarufu.

“Huyu msimamizi wa miradi ya ujenzi amerudi kazini,” Ng’ang’a ambaye si muongeaji sana mitandaoni aliandika.

Mama huyo ambaye miezi kadhaa iliyopita alichapisha mswada wake wa kitabu akielezea maisha yake kama mama kaunti kwa miaka 10 alijipata katika gumzo wiki chache zilizopita baada ya mumewe wa sasa, mwanamuziki Juliani kudokeza kwamba amezoroteka kimfuko na alikuwa anahitaji msaada wa angalau kumnunulia mwanawe nepi.

Ng’ang’a na aliyekuwa gavana wa Machakos Alfred Mutua walitengana mwezi Oktoba mwaka jana baada ya kudumu pamoja kwa zaidi ya miaka 10 na kufungua biashara za pamoja zenye thamani ya mamilioni.

Hajawahi zungumzia kilichomfanya kumbwaga gavana kwa ajili ya kijana mwanamuziki kutoka mitaani tu ila mwanamuziki Juliani wiki tatu zilizopita alitoa upenyo kiasi vile alivyopatana na Ng’ang’a na kumtwaa kutoka kwa gavana.

“Nilikuwa celibate wakati huo ata sikutaka stori ya manzi ju nilikuwa mahali poa sana. Lakini vitu vilichukua mkondo tu vile inafaa. Baadae aliniambia kusema kweli hivi ndio kuko, mimi siko hapo. Mimi nilisema sikuwa najua nilidhani sisi ni mabeshte tu,” Juliani alisema katika mahojiano na kituo kimoja cha redio humu nchini.