Daddy Owen amjibu shabiki aliyemkejeli kwa kutaka kuoa msichana wa kijijini

Daddy Owen alitangaza kuwa na shinikizo la kuwa na familia

Muhtasari

• Haya yamejiri baada ya Daddy Owen kufunguka kuwa na shinikizo la kuoa msichana wa kijijini kwa kuwa na hofu ya kutopata mtoto mwengine.

Image: INSTAGRAM// DADDY OWEN

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Daddy Owen amemjibu shabiki aliyemkejeli kwa kutaka kuoa msichana wa mashambani.

Katika Instastory zake, Daddy Owen alipakia screenshot ya taarifa za 'The Star' iliyotangaza mpango wa mwimbaji huyo.

Shabiki huyo alikuwa ametoa maoni yake katika chapisho hilo.

"Baada ya kujihusisha kimapenzi na wasichana wa jijini?" Shabiki huyo alisema.

Daddy Owen alikuwa ameshtushwa na maoni ya shabiki huyo mpaka kuchukua hatua ya kuchukua screenshot na kupakia mtandaoni.

"Kwa sababu ya nini? Mbona mko hivi lakini?" mwimbaji huyo alisema.

Haya yamejiri baada ya mwimbaji huyo kufunguka kuwa na shinikizo la kuoa msichana wa kijijini kwa kuwa na hofu ya kutopata mtoto mwengine.

Katika mahojiano yake na Word Is alisema kuwa ana wasiwasi kwamba umri wake unaendelea kusonga na bado hana familia yake.

Alisema kuwa mama yake ndiye aliyemshinikiza kutafuta mke ili awe na familia.

“Ananiambia hata niajiri mtu ili tu niache kutembea peke yangu nyumbani ana wasiwasi kwamba ninaishi peke yangu, natembea peke yangu, ” mwimbaji huyo wa takriban miaka 40 alisema.

Owen alisema kuwa licha ya kuwa na pesa, anahisi kuwa bado hajakamilika mpaka pale atakapopata mtu.

Hata hivyo, alieleza kuwa ana hofu ya kuwa akijitosa kwenye mahusiano au ndoa haitafaulu kama ndoa yake ya awali.