Fahamu msukumo wa Daddy Owen kutafuta msichana wa kijijini 'kienyeji'

Daddy Owen alifichua msukumo wake wa kutafuta msichana wa kijijini kuwa Rais Ruto na mkewe

Muhtasari

• Owen alijibu huku akipakia picha ya Rais William Ruto na mke wake Rachel Ruto na kusema kuwa wawili hao ni himizo lake.

Image: INSTAGRAM// DADDY OWEN

Mwimbaji wa nyimbo za injili Daddy Owen alifichua sababu yake ya kutaka kuoa msichana wa kijijini.

Katika kipindi cha maswali na majibu Instagram, shabiki alimuuliza ni kwa nini anatafuta msichana wa kijijini na sio mjini.

Owen alijibu huku akipakia picha ya Rais William Ruto na mke wake Rachel Ruto na kusema kuwa wawili hao ni himizo lake.

Picha hiyo aliyopaka ni ya rais na mkewe katika enzi zao za zamani walipokuwa wakichumbiana.

Rais William Ruto na mke wake
Image: DADDY OWEN INSTAGRAM

Vile vile katika instastory zake, mwimbaji huyo alivutiwa na shabiki mmoja aliyesema hajui maana ya 'kienyeji.

Shabiki huyo alimuuliza Owen maana ya jina hilo ambalo amekuwa akieneza kama sifa ya mwanamke anayehitaji kuwa mke wake.

"Watu humaanisha nini wakimwita mtu kienyeji? Kuna siku niliitwa kienyeji kisha watu wakaanza kucheka," binti huyo aliuliza.

Owen alisema kuwa amevutiwa kwa kuwa binti huyo hakua mjuaji kama mabinti wengine wa mtandaoni wanaofahamu kila kitu.

Alisema kuwa huenda binti huyo ndiye atakayechagua miongoni mwa wanawake wengine waliotaka kuchumbiana naye.

"Wewe ndiye unayefaa kunitafuta, unasema hujui hata maana ya kienyeji?? Lo!" mwimbaji huyo alisema.

Zaidi ya hayo, Owen aliulizwa ni kwa nini anataka mwanamke mweusi kuwa chaguo lake la mke kisha akasema kuwa roho yake inavutiwa na wanawake wenye rangi hiyo.

Daddy Owen aliweka wazi kuwa ingawa anataka mwanamke wa kijijini, mwanamke huyo asiwe kwenye mtandao wowote wala kuwa na mtoto.

Aliyekuwa mpenzi wa Simple Boy, Pritty Vishy, alitoa ombi kwa watu wanaoweza kumfikia msanii huyo kumwambia kwamba yupo radhi kuwa mke wake kwani ana sifa za kienyeji.

Msanii huyo alijibu ombi la Vishy na kumwambi kwamba anapaswa kusubiri kwani foleni ni ndefu sana na kuwa bado hajafikiwa.

"Huyu mwambieni line ni ndeefu,hajafikiwa bado..lakini kama marathon tutazawadi kila mmoja atakaye vuka laini," Alisema.