Mimi ni kienyeji pro max tafadhali nioe - Pritty Vishy amwambia Daddy Owen

Pia napenda maombi sana - Vishy

Muhtasari

• Mimi si rangi ya mkorogo kwa sababu sijui mtu anakuwa mkorogo aje. - Vishy.

Pritty Vishy amtaka Daddy Owrn kumuoa
Pritty Vishy amtaka Daddy Owrn kumuoa
Image: Instagram

Mshawishi wa mitandao ya kijamii Pritty Vishy, ​​ambaye jina lake halisi ni Purity Vishenwa, amejitolea kuwa mke kienyeji wa Mwimbaji wa nyimbo za Injili Daddy Owen.

Hii ni baada ya msanii huyo hivi majuzi kutangaza kuwa anatafuta mwanamke wa kumuoa na kusema kwamba kigezo kikubwa ni mwanadada huyo kuwa wa kutoka mashambani na wala si wa mjini.

Vishy ambaye anajiita malkia wa kutoka mashambani ametoa ombo kwa watu wanaoweza kumfikia msanii huyo kumwambia kwamba yupo radhi kuwa mke wake kwani tayari kigezo cha kuwa kienyeji tayari anacho.

 

“Na si mtu amwambia Daddy Owen kwa niaba yangu kuwa nipo singo na bila vipodozi mimi ni mweusi wa asili. Mimi si rangi ya mkorogo kwa sababu sijui mtu anakuwa mkorogo aje. Pia napenda maombi sana, ifikie Daddy Owen,” Vishy aliandika kwenye instastory yake.

Pritty alikua maarufu katika duru za burudani kufuatia uhusiano wake na mwanamuziki Stivo Simple Boy.

Daddy Owen, 40, alikuwa amefichua kuwa alikuwa kwenye shinikizo la kuoa tena.

“Natafuta mwanamke wa dhati wa kuchumbiana naye na kuoa. Natafuta mwanamke mwenye ngozi nyeusi, mwenye maombi sana. Anapaswa kuwa kutoka kijijini,” alisema.

Daddy Owen, aliyezaliwa kama Owen Mwatia, alisisitiza: “Ndiyo sababu mimi hutembelea mara kwa mara na kuendesha miradi kijijini. Nataka kupata mwanamke kutoka huko. Sitaki kuchumbiana na mtu aliyezaliwa mjini.”

Mwimbaji huyo aliongeza kuwa mwanamke huyo anapaswa kuwa na umri wa miaka 20 hadi 30 na lazima awe amemaliza shule ya upili.

“Nataka aliyesoma. Anaweza kuwa kienyeji (mwanamke wa kimila) lakini aliyeenda shule, hata aliyemaliza kidato cha nne. Afadhali awe na umri wa miaka 20 na 30 ya awali," aliongeza.

Hata hivyo, Owen ana hofu yake kufuatia uhusiano wake wa zamani.

“Sijajiandaa kwa vile naelewa si uamuzi wangu peke yangu, nahitaji kuwa na mtu. Kufanya kitu chochote na mtu mwingine kunaweza kukaibua kumbukumbu za uhusiano wangu wa awali. Mimi ni kama, nitamtendea vizuri au nitakuwa kwenye shinikizo sawa na uhusiano ukaisha tena?" Aliuliza.

Kufuatia talaka yake kutoka kwa aliyekuwa mke wake Farida, Daddy Owen amekuwa akiishi peke yake. Katika mahojiano yaliyopita kwenye vyombo vya habari, mwanamuziki huyo alizungumzia ndoa yake iliyokuwa na ugumu na kufichua kuwa ilikuwa na misukosuko na ilichangia mfadhaiko wake.