Aslay aibuka na filamu ya maisha yake baada ya kusainiwa na lebo ya Sony Music

msanii huyo alidhihirisha furaha yake baada ya kujinafasi kimkataba na lebo hiyo kubwa kabisa ya miziki duniani.

Muhtasari

• Ni Furaha leo kuwatangazia kuwa nimeingia rasmi kwenye familia kubwa na bora ya Sony Music. - Aslay.

• Kwa upande wao, Sony walifurahia kumpa mkataba Aslay na kusema kuwa ni nyongeza katika nia yao ya kuingia soko la muziki wa Afrika Mashariki.

Msanii Aslay apata mkataba na lebo ya Sony
Msanii Aslay apata mkataba na lebo ya Sony
Image: Instagram

Msanii Alsya kutoka Tanzania amejinyakulia mkataba na rekodi lebo ya kimataifa ya Sony.

Rekodi lebo hiyo ya kimataifa ilidhibitisha hilo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii na kusema kwamba mkataba huo ni hatua kubwa sana kwao kupenya katika soko la muziki wa Afrika Mashariki.

“Sony Music Africa yasaini Mkataba wa Kimataifa na staa wa Afrika Mashariki Aslay. Karibu kwa Familia. Aslay ana vibao vingi chini ya jina lake na amefanya kwenye jukwaa lukuki barani Afrika, ameweza kuchonga nafasi yake katika anga ya Afrika Mashariki na kupendwa na vijana na wazee kwa muziki wake unaohusiana na kutoka moyoni. Hii ni fursa nzuri, si kwangu tu, bali kwa muziki wa Bongo Flava, ninaoupenda sana,” Sony waliandika na kumtaja Aslay kwenye chapisho hilo.

"Ni Furaha leo kuwatangazia kuwa nimeingia rasmi kwenye familia kubwa na bora @sonymusicafrica @sonymusicea kwenye safari yangu ya muziki hasa kufika katika anga ya kimataifa.Wapenzi wa muziki wangu, ni wakat wa kukaa tayari tunaenda kimataifa sasa," Aslay alidhihirisha furaha yake pia.

Msanii huyo baada ya kusainiwa anatarajia kuachia moja ya filamu yake ya kuelezea mashabiki wake safari yake ya muziki wa Bongo, filamu ya kihalisia inayokwenda kwa jina ‘Mimi ni Bongo Fleva’

Filamu hiyo ya kibinafsi na ya kufungua macho itakuwa na sehemu tano za safari ya muziki ya msanii huyo ikifuatiwa na wimbo wake wa kwanza ambao unaashiria mwanzo wa safari yake mpya ya muziki.

Sehemu ya kwanza itamuona Aslay akifunguka na kusimulia historia ya maisha yake kwa mtazamo wake, sauti yake kwenye jukwaa lake.

 Msanii huyo ambaye alikuwa katika kikundi cha Yamoto Band na wenzake Mbosso, Enock Bella na Beka Flavour kabla ya kusambaratika miaka michache iliyopita, amekuwa mkimya kwenye muziki jambo ambalo liliibua wasiwasi kutoka kwa mashabiki wake.

"Ni muda mrefu umepita, mengi yalizungumzwa lakini sasa ni wakati sahihi wa Mimi kuzungumza. Subscribe kwenye YouTube Channel yangu YouTube.com/aslay na Facebook channel yangu facebook.com/aslayofficial , nimekuandalia majibu ya maswali yote uliokuwa ukitaka kufahamu kutoka kwangu," aliandika kwenye kionjo cha filamu hiyo.