Tafadhali nioe kwa harusi - Diana Marua amuomba Bahati

Baadhi ya watu walimshambulia kwa kusema kuwa hana haja ya kubembeleza harusi kutoka kwa mtu ambaye amemzalia watoto watatu.

Muhtasari

• Hii ni mara ya pili ambapo Bahati anamvuta msanii wa Ohangla Prince Indah kwenye collabo.

• Collabo ya kwanza iliyowakutanisha wasanii hao ilikuwa ile ya Adhiambo.

Wapenzi Bahati na Diana
Wapenzi Bahati na Diana
Image: Instagram

Mwanablogu wa YouTube ambaye pia ni msanii wa kutema mistari, Diana Marua amemuomba kwa upole na unyenyekevu mumewe Bahati Kioko kumuoa rasmi kwa kufunga ndoa takatifu naye.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diana Marua alipakia bango la kutangaza ujio wa ngoma mpya ambayo ni collabo Bahati kwa mara nyingine amemshirikisha msanii maarufu wa Ohangla, Prince Indah. Aliandika kwenye bango hilo ombi lake moja kwa mumewe Bahati kwa kumtaka amuoe kabisa ili aweze kucheza na kufurahia wimbo huo kwa jina ‘Abebo’ akiwa anatembea kwenye zulia la maharusi wakielekea mbele ya madhabahu kula yamini ya kuishi milele kama mwili mmoja kwa upenda wa Muumba.

“Mpenzi wangu Bahati tafadhali nioe, nataka kutembea kwa zulia la maharusi nikifurahia mandhari ya huu wimbo,” Diana alimuomba Bahati.

Hii ni mara ya pili ambapo Bahati anamvuta msanii wa Ohangla Prince Indah kwenye collabo, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka jana walipofanya kweli kwenye kichupa cha ‘Adhiambo’ wimbo uliopata mapokezi mazuri na mashabiki wa muziki wa Kenya.

Diana na Bahati walikuwa awali wamedokeza kuwa Novemba 30 ilikuwa ni harusi yao haswa baada ya kupakia picha ya kutambulisha wimbo huo akiwa amevalia shela jeupe la bibi harusi.

Wengi walikuwa wanasubiria harusi kumbe ilikuwa ni uzinduzi wa kibao hicho cha Abebo ambapo kwa siku moja tangu kuachiwa, goma tayari lina watazamaji karibia laki tatu kwenye jukwaa la kupakuwa miziki la YouTube.