Nakwenda kumfungulia Kajala kesi ya kumharibia muda Harmonize - Mwijaku

Mwijaku alimtaja Kajala kama mwanamke mnafiki ambaye ameharibu muda wa Harmonize kwa zaidi ya miezi 5 iliyopita.

Muhtasari

• Mwijaku alimtaja Kajala kama mwanamke mnafiki ambaye ameharibu muda wa Harmonize kwa zaidi ya miezi 5 iliyopita.

• Kajala na Harmonize waliachana mwishoni mwa wiki jana.

Mwijaku atishia kumshtaki Kajala kwa kumharibia muda Harmonize
Mwijaku atishia kumshtaki Kajala kwa kumharibia muda Harmonize
Image: Maktaba

Mtangazaji mbwatukaji Mwijaku amemgeuka Kajala na sasa anadai kuwa ataelekea mahakami kumfungulia kesi ya ulaghai na kumharibia msanii Harmonize muda wake kwa zaidi ya miezi 5.

Mwijaku alipakia video Harmonize akimvisha pete Kajala kule Milimani city mwezi Juni ambapo yeye ndiye alikuwa mshereheshaji mkuu na kusema kuwa alimuuliza Kajala kurudia maneno yake kwa Harmonize.

Kajala anasikika akirudia maneno yake kwa Harmonize akimpa hakikisho kuwa atampenda leo, kesho na hadi milele.

Mwijaku alisema aliona Kajala alikuwa mnafiki kwa maneno yake na ndio maana akamuomba arudie huku akijifanya kuwa hakusikia mara ya kwanza.

Hapa nilivo mwambi RUDIA nilitaka kujihakiki je hii inatoka ndani ya moyo wake? Na alivyokuwa mpumbavu akarudia nyoko yake nikajua ni MNAFIKI HUYU mwanamke,” Mwijaku aliandika kwenye video hiyo.

Alisema kuwa sasa anasalia na hatua ya kuelekea mahakamani kumfungulia Kajala kesi ya kuharibu muda na mali ya msanii wa watu Harmonize na mwisho wa siku kukiuka maneno yake kuwa atampenda muda wote.

“Nakwenda kufungua kesi ya madai mahakamani kesho . Ya kumpotezea muda msanii,” Mwijaku alisema.

Mtangazaji huyo wa redio awai alikuwa rafiki wa karibu sana wa Harmonize lakini hapa kati wakaja kugeukiana katika kile alianza kunadi kuwa Harmonize anatoka kimapenzi na Kajala pamoja na bintiye Paula tena kweney kitanda kimoja.

Lakini tangu Kajala atangaze kumuacha Harmonize, Mwijaku ameonekana kujileta kwangu kwangu kwa Harmonize huku juzi pia akipakia video yake kwenye Instagram na kumsifia kwa utunzi mzuri wa video wimbo wa video mpya ya ‘Mwenyewe’ aliyoitoa Ijumaa.

“Napenda hadithi ya video hii ..! Haijalishi unayo pitia ila mpumbavu wewe kwenye ubunifu utakufa na hiyo sifa yakoo. Najivunia nawe japo sijui unayo yapitia kikubwa usife bongo fleva inakuhitaji NYOKO wewe,” Mwijaku aliandika.