Muache Whozu tuone kama ataishi - Mwijaku amshauri Wema Sepetu

Alisema kuwa kijana huyo amejisahau kwa Sepetu hata akipigiwa simu hachukui.

Muhtasari

• "Kama vipi hebu mmwage tuone kama ana moyo wa ustahimilifu kuishi bila Wema,” Mwijaku alimwambia Sepetu.

Mwijaku amtaka Wema kumuacha Whozu
Mwijaku amtaka Wema kumuacha Whozu
Image: Instagram

Mtangazaji mropokaji Mwijaku Burton ametumia kisa cha Kajala kumuacha Harmonize baada ya kumfyonza mali yake, na kumshauri mwigizaji mkongwe Wema Sepetu asjie akafanay hivyo kwa mpenzi wake mdogo mwanamuziki Whozu.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mwijaku alimwambia Sepetu kuwa asidhubutu kumfanyia hivyo mtoto wa watu Whozu kwani atashtukia kumpata amelazwa mochwari kama gogo lisilo na uhai wala pumzi.

“Wema nakuombea dua usije ukafuata nyayo za Kajala. Maana huyu Whozu utamkuta mochwari ukimuacha. Kijana kajisahau hata akipigiwa simu hapokei, najua ni kwa sababu ya utamu unaompa. Kama vipi hebu mmwage tuone kama ana moyo wa ustahimilifu kuishi bila Wema,” Mwijaku alimwambia Sepetu.

Gumzo la kuachana kwa Kajala na Harmonize limeonekana kumgusa pakubwa Mwijaku ambaye sasa ameonekana kumtetea Harmonize vikali akisema kuwa Kajala ni mhitimu wa utapeli ambaye amehakikisha kujilimbikizia zawadi za thamani kubwa kutoka kwa Harmonize kabla ya kumuacha hoi.

Baadhi wanahisi kuwa Kajala na Harmonize bado wapo pamoja ila ni kiki tu wanajaribu kutafuta mitandaoni na wengine wakisema ni kweli huenda wawili hao wamefikia tamati ya mapenzi yao.

Mpaka sasa, Kajala ndiye pekee amedokeza kuachana na Harmonize lakini msanii huyo hajazungumza wala kuonesha dalili yoyote ya kuachana naye kwani anazidi kufanay mambo yake kawaida.

Wema Sepetu alitangaza kutoka kimapenzi na Whozu miezi michache iliyopita lakini baadae akasema kuwa haoni uhusiano huo ukienda mbali hadi kufikia ndoa.