Kinuthia aibua maswali mengi kuliko majibu mitandaoni akijiita 'baby girl'

Alikuwa amevalia nguo za manjano na kusema kuwa ni mtoto wa kike akisherehekea kuzaliwa kwa Yesu.

Muhtasari

• “Mtoto wa kike akisherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo,” Kinuthia aliandika.

kELVIN KINUTHIA
kELVIN KINUTHIA
Image: INSTAGRAM

Sehemu ya wanamitandao ya kijamii imechukizwa na hatua ya mwanablogu wa Tiktok, Kelvin Kinuthia kujiita mtoto wa kike licha ya yeye kuwa wa kiume.

Kinuthia ambaye umaarufu wake ulitokana na umbile lake la kike na kuvalia mavazi ya kike pamoja na kujipodoa alipakia picha akiwa amevalia nguo za kike rangi ya manjano na kujiita kama mtoto wa kike ambaye alikuwa anasherehekea kuzaliwa kwa Yesu, siku ya Krismasi.

“Mtoto wa kike akisherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo,” Kinuthia aliandika.

Japo kwa mara kadhaa mwanamitindo huyo amekuwa akikwepa swali la kuweka wazi jinsia yake, wengi bado wanaamini ni mwanaume kutokana na jina lake na kumtaka kutojificha katika mavazi ya kike kujidhalilisha.

Hata hivyo kuna wale ambao wanamiini kuwa huenda Kinuthia ni shoga lakini haijawahi kudhibitishwa bayana.

“Ati baby girl, ni sawa basi krismasi njema mtoto wa kike,” Akoth Oduor alimwambia kwa kejeli.

“Aliyemroga Kinuthia bado yuko hai. Kijana amehangaika sana,” Dennis Too alisema.

“Unahitaji huyo  Yesu ili akusaidie ubadilike kutoka baby girl na kuwa mwanaume kamili. Hii ni aibu,” mwingine alimwambia.

“Kwa vile unavyoelekea sijui tukuite Shiru ama?” Irene Trizah alimuuliza.

Miezi kadhaa iliyopita Kinuthia alisema kuwa alikuwa anatafuta mtu japo hakusema ni mtu yupi anataka na hakuweza wazi kama ni mwanaume ama mwanamke anataka.

Fununu za uwezekano wa kuwa shoga ziligonga vichwa vya habari alipoonekana kwenye video wakiwa wamepakatana na mwanablogu mwingine kwa jina Mtumba Man picha ambazo walizifuta muda mchache baadae baada ya watu kuwatupia lawama za kila aina.