Mwanatiktoker kumlipa Nonini shs.1M kwa kukiuka hakimiliki

Nonini alidai kuwa Brian alitumia wimbo wake bila idhini yake.

Muhtasari

• Nonini alieleza kuridhishwa kwake na matokeo ya kesi hiyo na akaeleza furaha yake kwenye mitandao ya kijamii.

Nonini alelekea mahakamani kuishtaki Synix
Nonini alelekea mahakamani kuishtaki Synix
Image: Instagram

Mwanamuziki wa Kenya Nonini, Hubert Nakitare, ameshinda kesi ya ukiukaji wa hakimiliki dhidi ya mshawishi wa mitandao ya kijamii Brian Mutinda.

Mnamo Machi 23, 2023, Mahakamai ya Milimani ilitoa uamuzi uliounga mkono Nonini, ikamwamuru Mutinda kumlipa msanii huyo fidia ya jumla ya Shilingi milioni moja na pia kuondoa video iliyoleta kuzuka kwa  kesi hiyo kutoka kwa mitandao yote ya kijamii.

Kesi ya Nonini iliwasilishwa baada ya Mutinda kuangazia wimbo wake maarufu We Kamu katika tangazo la video ambalo lilikuza runinga mpya zaidi za chapa ya Syinix. Nonini alisema wimbo wake uliovuma sana aliutumia bila ridhaa yake wala idhini yake, hivyo kumfanya apelekwe mahakamani mwaka jana.

Nonini alieleza kuridhishwa kwake na matokeo ya kesi hiyo na akaeleza furaha yake kwenye mitandao ya kijamii

"Leo, Machi 23, 2023, itaingia katika historia (Mwaka wa Jordan) na ni ushindi kwa tasnia ya muziki ya Kenya ,Mgenge 2 dhidi ya watu waliotumia wimbo wangu Wee Kamu kusukuma bidhaa. #HakimilikiItaheshimiwa.” Nonini  alisema.

Mtuhumiwa alikuwa pia na amehusishwa na kesi kadhaa za ukiukaji wa hakimiliki zilizoendelea kwa miaka.

Nonini alisema uamuzi wa mahakama ulikuwa umeweka mfano ambao utasaidia kulinda haki za wasanii nchini Kenya. Uamuzi katika kesi hii unakuja wakati wakili wa burudani na haki miliki Liz Lenjo amewaonya waundaji wa maudhui  ya kutumbuiza kutafuta kibali kabla ya kutumia haki miliki ya mtu mwingine.

Alibainisha kuwa chapa zinazoshirikisha washawishi lazima zihakikishe kuwa zina haki zinazohitajika za kutumia mali miliki kama vile muziki, picha, au mali nyingine yoyote ya kiakili, ili kuepuka mizozo ya kisheria.