Zuwena Platnumz achora tattoo ya Diamond kwenye mkono wake (Video)

Zuwena alisema kuwa anampenda sana Diamond na kuchora tattoo yake ni njia moja ya kulinda nadhiri ya kumkumbuka milele.

Muhtasari

• “Diamond Platnumz milele na milele,” Zuwena aliandika kweney video hiyo akiwa pia ameshika picha ya msanii huyo.

Zuwena achora tattoo ya Diamond
Zuwena achora tattoo ya Diamond
Image: Instagram//ZuwenaPlatnumz

Recho Elias, mwanadada ambaye nyota yake ya jaha ilipata mwanga ghafla baada ya kucheza kama vixen kwenye video ya wimbo wa msanii Diamond Platnumz, Zuwena kwa mara nyingine tena amefanya jambo kubwa lisilotarajiwa na wengi kama njia moja ya kuonesha shukrani zake kwa Diamond.

Zuwena Platnumz kama anavyojiita mitandaoni amejichora tattoo ya uso wa Diamond kwenye mkono wake wa kushoto, akisema ni kitu alichokifanya kama kuendelea kumkumbuka na kumuenzi Diamond kwani ndiye alimuokota kutoka kizani na kumleta kwenye mwanga.

“Diamond Platnumz milele na milele,” Zuwena aliandika kweney video hiyo akiwa pia ameshika picha ya msanii huyo kwenye mkono huo huo aliouchora tattoo kubwa ya uso wake.

Mpaka sasa tangu mwaka 2023 kuanza, Diamond ametoa nyimbo tatu lakini hiyo ya Zuwena imekuwa pendwa kwa sehemu kubwa tu ya mashabiki wake, haswa wakimsifia mwanadada huyo kwa jinsi alivyoivalia ‘character’ ya Zuwena na kuwasilisha ujumbe wa wimbo huo kwa ufasaha.

Zuwena katika mahojiano baada ya ngoma hiyo kumtambulisha kwa watu wengi, alisema kuwa hatokuja kukaa amsahau Diamond kwani kabla ya kuonekana kweney video hiyo alikuwa na maisha ya kuunga unga na kubahatisha.

Alisema kuwa Diamond alimlipa vizuri sana kucheza kama vixen kwenye ngoma hiyo, akifichua kutia kiindoni kitita cha milioni 17 pesa za Kenya.

Hata hivyo, Zuwena hakusahau maisha ya kubahatisha aliyokuwa akiyapitia kwani wiki kadhaa baadae alionekana akigawa chakula na bidhaa zingine za msaada kwenye boma moja la kuwalea watoto mayatima, akisema kuwa njia pekee ya kuendelea kupata thawabu ni kurudisha mkono kwenye jamii ya wale ambao hawana uwezo na wenye uhitaji maalum.