Sisi ni marafiki tu!! Butita azungumzia uhusiano wake na Sadia

Mimi na Sadia hatujawahi chumbiana, sisi ni marafiki tu na washirika wa biashara.

Muhtasari

• Wawili hao walikuwa wamezua tetesi za uchumba na hivi majuzi ilionekana kana kwamba kulikuwa na matatizo katika uhusiano wao.

• Mimi na Sadia hatujawahi chumbiana, sisi ni marafiki tu na washirika wa biashara.

Eddy Butita na Sadia
Eddy Butita na Sadia
Image: HISANI

Mchekeshaji maarufu Eddie Butita amezuka kuweka mambo sawa kuhusu uhusiano wake na  Sadia.

Wawili hawa wameonekana pamoja mara kadhaa na hivi majuzi walionekana wakiwasili pamoja kwenye helikopta katika harusi ya Akothee.

Wawili hao walikuwa wamezua uvumi kuwa wanachumbiana na hivi majuzi ilionekana kana kwamba kulikuwa na uchachu katika mahusiano yao.

Sadia alichapisha video kwenye akaunti yake ya Instagram akionekana kufurahia muda wake na mwanaume mwingine. Mwanamume huyo anafahamika kama Moyazy, mwanamuziki Marekani.

Sadia alichapisha video zao wakicheza kwenye vilabu na hata amedokeza kuwa anatayarisha wimbo wa kumuimbia mpenzi wake.

Mashabiki walionekana kumsikitikia Butita kwa kuachwa na Sadia.

Butita akizungumza na mtangazaji Ankali Ray alifafanua hali ya uhusiano wao.

"Hatujawahi kuchumbiana na sisi ni marafiki tu na washirika wa biashara ambao wanafanya kazi pamoja," Butita alisema.

Mcheshi huyo aliongeza kuwa wawili hao hawajawahi kukiri wazi kuwa wanachumbiana na Sadia.

"Watu walituona pamoja na wakajiamulia kwamba tunachumbiana, hakuna aliyeuliza."

Butita alisema bado hajaoa na anatafuta mchumba na kuwa Sadia ana haki ya kupakia mchumba wake.

Alipoulizwa kuhusu yeye na ex wake kuwahi kurudiana, alisema hilo halingewezekana.

Aidha mchekeshaji huyo alisema akipata mpenzi ataujulisha umma lakini hadi sasa bado hana mchumba.