Sababu za watu maarufu kutokezea na mitindo mipya ya nywele

Kwenye mtandao mastaa mbalimbali walionekana wakiwa na mitindo mipya ya nywele ambayo iliweza kuwashangaza mashabiki.

Muhtasari

• Wengine walikuwa na nywele za rasta huku wengine wakiwa bila nywele ila sasa wanaonekana na mtindo mpya wa nywele.

Sababu za watu maarufu kunyoa nywele zao zilizokuwa kama nembo ya utambulisho
Sababu za watu maarufu kunyoa nywele zao zilizokuwa kama nembo ya utambulisho
Image: Instagram

Kwenye mtandao mastaa mbalimbali walionekana wamepakia picha wakiwa na mitindo mipya ya nywele ambayo iliweza kuwashangaza mashabiki.

Wengine walikuwa na nywele za rasta huku wengine wakiwa bila nywele ila sasa wanaonekana na mtindo mpya wa nywele.

Kwani mastaa ambao walikuwa na nywele za rasta wengi wao walinyoa na hivyo basi walieleza sababu kuu ambazo zilifanya wao kubadilisha muonekano.

Lupita Nyong'o (2023) - Alishrutika kunyoa baada ya kutuma maombi ya kuigiza kwenye filamu mpya ya Dora Milaje.

Thee Pluto (2022) - Alinyoa rasta zake baada ya kuahidiwa milioni 1 iwapo angefanya kuthubutu kunyoa .

Ivy Namu (2022) - Alishrutika kunyoa ili kuukaribisha mwaka wa 2023 kwa muonekano mpya

Nadia Mukami (2022) - Alinyoa baada ya upara wake kuanza kuonekana.

Carol Sonie (2022) - Alinyoa nywele ili aone kama mambo yake yatamwendea sawa.

Willis Raburu (2022) - Alinyoa ili kuthibitishia watu kuwa anaweza kufanya anachotaka.

Sean Andrew (2022) - Alinyoa rasta zake kwa kuwa alichoka kubeba uzito wake na vilevile kuhusishwa na jamii ya Warasta.

Willy Paul (2022) - Alinyoa rasta ili kubadilika na kuwa mtu mzuri aliongezea na kusema kuwa kwa kunyoa aliondoa dhambi.