Manzi wa Kibera amtema mchumba wake mzee, afichua sababu

Mwanasoshalaiti huyo alisema wanamitandao walimuonyesha chuki huku wengine wakimrushia cheche za matusi.

Muhtasari

• Manzi wa Kibera aliyeonekana kujawa na huzuni alitangaza kuwa yeye na mzee hawako pamoja tena.

Manzi wa Kibera na mchumba wake
Image: INSTAGRAM// MANZI WA KIBERA

Mwanasoshalaiti Sharifa Sharon Wambui almaarufu Manzi wa Kibera amefichua ametengana na mchumba wake mzee.

Kwenye instastori zake, Manzi wa Kibera aliyeonekana kujawa na huzuni alitangaza kuwa yeye na mzee hawako pamoja tena.

"Mimi na mzee hatuyuko pamoja tena," alisema mwanasosholaiti huyo na kumalizia kwa emoji za huzuni.

Manzi wa Kibera kutengana na Mchumba wake mzee
Manzi wa Kibera kutengana na Mchumba wake mzee
Image: Instastory

Mmoja kati ya mashabiki yake alimuuliza sababu ya kutengana na mzee na akaeleza kwamba ataelezea zaidi baadaye kwa kuwa ni hadithi ndefu.

Mwanasoshalaiti huyo alielezea kuwa amewaza kuvunja mahusiano na mpenzi huyo wake wa miaka 66 kutokana na chuki na unyanyasaji iliyoko mtandaoni.

Aliendelea kueleza kuwa wanamitandao wengi walimuonyesha chuki huku wengine wakimrushia cheche za matusi katika sehemu ya maoni na alisema kuwa watu wengi walikuwa wakipinga uhusiano wake na mchumba wake mzee.

Wiki chache zilizopita, katika video zilizovuma kwenye mitandao ya kijamii, mwanasosholaiti huyo asiyepungukiwa na drama alionekana akiwa ameandamana na mpenziwe kabla ya mzee huyo kupiga magoti na kumuomba wafunge ndoa.

Baadaye, mwanasosholaiti huyo alidokeza kufunga pingu za maisha na mchumba huyo wake katika siku za hivi karibuni.

Licha ya kuchumbiana kwa muda mrefu, kipusa huyo anayezungukwa na sarakasi nyingi maishani hata hivyo amebainisha kwamba anasubiri ndoa rasmi ili kumuonjesha mchumba huyo wake zawadi ya ndoa aliyomhifadhia.