Diamond huwa anasaini wasanii WCB mkataba miaka 10, meneja wake aelezea kwa nini

Babu Tale alisema baada ya Mavoko, Harmonize na Rayvanny kuondoka kwa kufuatana, uongozi wa WCB uliingiwa na hofu na ndio maana hawajakuwa na haraka ya kutafuta wasanii wapya.

Muhtasari

• Mwanzo, Tale alianza kwa kuzungumza ni kwa nini Platnumz amechukua muda mrefu kuwasaini wasanii wengine.

Meneja wa Diamond, Babu Tale amefunguka ni kwa nini wasanii wanafungwa WCB kwa mikataba ya miaka 10
Meneja wa Diamond, Babu Tale amefunguka ni kwa nini wasanii wanafungwa WCB kwa mikataba ya miaka 10
Image: Instagram

Meneja wa Diamond ambaye pia ni mbunge wa Morogoro Kusini Babu Tale kwa mara ya kwanza amenyoosha maelezo kuhusu ni kwa nini msanii Diamond anawapa wasanii wapya mikataba ya miaka mitano hadi 10.

Katika mahojiano na Millard Ayo, Tale alifichua kwamba wasanii wapya ambao wamesainiwa katika lebo ya WCB Wasafi tangu uzinduzi wake, wote hawakupewa mkataba unaozidi miaka 10, na kuelezea ni kwa nini.

Mwanzo, Tale alianza kwa kuzungumza ni kwa nini Platnumz amechukua muda mrefu kuwasaini wasanii wengine ili kuchukua nafasi ya wale walioondoka akiwemo Rich Mavoko, Harmonize na Rayvanny.

“Kumpa msanii mkataba ni hatua. Diamond anachunguza vitu vingi sana. Kuondoka kwa wasanii kulitupatia hofu zile za kuangalia huyu, aah huyu… tulikuwa tunasaini haraka unajua lakini tuliingia hofu.. huyu… ile hipo ile kama binadamu,” Tale alisema.

Alisema kuwa kinachowafanya kumpa mkataba msanii kwa miaka mirefu ni dhana kwamba msanii huwa hachipukii mara mja puh bali huchukua muda kupikwa, kufinyangwa na kutayarishwa kwa ajili ya kuteka anga za muziki, na katika hilo hela ndefu inahusika.

“Mikataba huwa ni miaka 10, mitano inategemea. Biashara ya muziki mtu huwa hakui kwa haraka, huwa anabobea mbele huko. Kwa mfano unaona Tetema ina kama miaka mitatu lakini anatitiga spika mpaka leo. Mikataba yote ni miaka 10,” Babu Tale alisema.

Mwaka jana baada ya Rayvanny kuondoka, kuliibuka shtuma mitandaoni baadhi wakisema kuwa mikataba ya WCB ni ya unyonyaji kwa wasanii.

Rayvanny alidaiwa kulipa shilingi bilioni 69 za Kenya ili kuvunja mkataba wake, miaka mitatu baada ya Harmonize pia kudaiwa kulipa takribani milioni 24 za Kenya kuuvunja mkataba wake Usafini.