Hatimaye Eric Omondi afichua uso wa bintiye kwa mara ya kwanza

Omondi alikuwa ameweka wazi kuwa kuona mtoto wake ni kima cha shilingi milioni 50

Muhtasari

• Miezi  mitatu iliyopita mchekeshaji Eric Omondi na mpenzi wake wa muda mrefu Lynn  walikuwa na hamu ya kutarajia mtoto wao wa kwanza.

Mtoto wa Eric Omondi
Mtoto wa Eric Omondi
Image: Facebook

Siku chache baada mchekeshaji na mwanablogu Eric Omondi kufichua kuweka wazi sura ya bintiye mitandaoni hatimaye ameweka  wazi sura ya bintiye wa miezi mitatu baada ya kuzaliwa kwenye ukurasa wake wa instagram.

Alhamisi  hii Eric alichapisha picha za bintiye kuonesha  uso wa bintiye, Kyla, kwa ulimwengu, Ufichuzi huo, uliogubikwa na matarajio  mengi kutoka kwa wafuasi wao  hakika umepokelewa vyema na wanablogu  wa mitandao.

Itakumbukwa miezi mitatu iliyopita kabla ya mwanawe kuzaliwa, Omondi alikuwa ameweka wazi kwamba asingeweka sura ya bintiye mitandaoni pasi na mtu kutoa kima cha shilingi milioni 50.

"Kufichua uso wa mtoto wangu haitakuwa rahisi," Omondi alisema. “Ili niweze kuonesha uso wa mtoto wangu, nitahitajika kulipwa Ksh 50 milioni. Atakayetoa kiasi hicho,  ndiye atakayeonyesha sura yake. Uso wa mtoto wangu ni adimu sana na wa thamani.”

 

Miezi  mitatu iliyopita mchekeshaji Eric Omondi na mpenzi wake wa muda mrefu Lynn  walikuwa na hamu ya kutarajia mtoto wao wa kwanza miezi michache baada ya kutangaza kuharibikiwa na mimba yao ya kwanza.