“Nimechoka, nataka mume!” Dacha asema wiki baada ya kutaja sifa ya mume wa ndoto zake

“Nataka mume. Nimechoka kuwaambia wanaume 20 jinsi siku yangu ilienda,” Sandra Dacha alisema kwa utani.

Muhtasari

• “Nataka mume. Nimechoka kuwaambia wanaume 20 jinsi siku yangu ilienda,” Sandra Dacha alisema kwa utani.

SANDRA DACHA
SANDRA DACHA
Image: FACEBOOK

Wiki moja baada ya kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii kufuatia hatua yake y kuorodhesha kwa ukamilifu vigezo na sifa za mwanamume wa ndoto zake, muigizaji Sandra Dacha sasa amedai kuwa amechoka kuwa bila penzi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Sandra Dacha alisema kwamba wakati umefika naye kupata mume wa kwake, akitania kuwa amechoka kuwadananya wanaume wengi jinsi siku yake ilienda, kila mmoja wao akifikiria kuwa ni yeye peke yake amejinafasi katika moyo wake.

“Nataka mume. Nimechoka kuwaambia wanaume 20 jinsi siku yangu ilienda,” Sandra Dacha alisema kwa utani.

Muigizaji huyo mnene aliyejibatiza jina la ‘Biggest Machine’ kama njia moja ya kukumbatia na kuyakubali maumbile yake aliyasema haya, ikiwa ni wiki moja baada ya kuweka wazi sifa za mwanamume atakayemkubali kuwa mumewe.

Katika mahojiano na K24, mama huyo wa mtoto mmoja alisema;

“Nataka mtu ambaye hana wivu,"

Dacha alichukua nafasi hiyo kuibua kumbukumbu jinsi mpenzi wake wa awali alimuacha kisa wivu.

"Mwanzoni mwa mwaka jana, mpenzi wangu wa zamani aliniacha kwa sababu nilinunua friji ambayo ni kubwa kuliko yake," alisema.

Kulingana na Sandra, sifa nyingine anayotafuta mwanamume ni utulivu wa kifedha.

"Sifa ya pili ninayotafuta kwa mwanamume ni mtu anayefaa kifedha," alisema

"Pia nataka mwanaume ambaye ananizingatia kikamilifu. Mtu anayeuliza juu ya matamanio yangu na matarajio yangu. Sitaki mtuu amezubaa tu.”