Polisi hatimaye wakubali DP Ruto kufanya mikutano Nyamira

Muhtasari

•DP Ruto akubaliwa kuweka mikutano katika kaunti ya Nyamira na polisi

•Mkutano wake wa wiki jana ulifeli baada ya polisi kuawanya wananchi na kudai hawakuwa na ruhusa kutoka kwa polisi

 

Ruto
Wiliam Ruto Ruto
Image: Maktaba

Hatimaye DP William Ruto amekubalishwa kufanya mikutano yake katika kaunti ya Nyamira Alhamisi ijayo hii ni baada ya mkutano wake wa awali kufeli baada ya polisi kukita kambi katika maeneo hayo na kuwatawanya wananchi.

Polisi walitumia vitoa machozi ili kuwatawanya watu katika shule za msingi za Kebirigo na Nyangoge.

Haya yalijiri baada ya vijana wawili kupoteza maisha yao katika eneo la Kenol kaunti ya Murang'a baada ya vurugu kutokea maeneo hayo.

 

Mbunge wa Mugirango Vincent Kemosi na muhubiri Richard Nyaribari jumanne waliomba ruhusa ili waweze kuweka mkutano na naibu rais ambapo walipewa ruhusa na polisi huku wakiambiwa watafanya kazi na polisi wa usalama katika eneo hio.

"Kama mkusanyaji utafanya kazi na polisi ili kuhakikisha haku na sheria imefuatwa wakati wa mkutano huo

utawajibika kama sheria itavunjwa na kama masharti hayatafuatwa wakati huo ."