- Ruto asema vitoa machozi havifai kuwa na karibu na kanisa au waumini
- Asema viongozi wanafaa kuheshimiana hata wanapotofautiana katika maoni
- Kibwana amesema magavana hawafai kukubali kutishwa
Naibu wa Rasi William Ruto amewataka viongozi kuwavumilia wenzao . Amesema ni vyema iwapo viongozi wataheshimu maoni na misimamo ya wenzao hata wanapotofautiana
“ Tushirikiane . Tunataka nchi ambayo sote tunaweza kutembea pamoja’ amesema Ruto
Alikuwa akizingumza siku ya jumapili katika kanisa la AIC huko Bomani ,Machakos
Naibu wa rais alikuwa ameandamana na gavana wa Makueni Kivutha Kibwana, wabunge Victor Munyaka (Machakos), Vincent Musyoka (Mwala), Nimrod Mbai (Kitui East), Aisha Jumwa (Malindi), Kimani Ichung’wa (Kikuyu), George Theuri (Embakasi West) na Nixon Korir (Lang’ata).
Ruto aliomba msamaha kwa niaba ya serikali kuhusu ghasia zilizoshuhudiwa katika maeneo ya Murang’a, Kakamega na Nyamira .
“ Hatufai kushuhudia mambo kama hayo katika nchi inayomtii mungu . vitoa machozi havifi kuwa karibu na kanisa au waumini’ amesema Ruto
Akiunga mkono wito huo wa Ruto ,gavana Kivutha Kibwana amesema viongozi na hasa magavana hawafai kukubali kutishwa kuchukua misimamo Fulani ya kisiasa .
“ Tuliipigania katiba hii kwa sababu tulijua itamchukulia kila mtu kuwa sawa.Hatujafurahi kuhusu jinsi mambo yanavyoendeshwa katika nchi hi’ amesema Kibwana
Gavana huyo wa Makueni amesema katiba ya sasa haiheshimiwi