Sonko atangaza kuchukua mapumziko ya miaka 10 kutoka kwa siasa

Muhtasari
  • Kwa sababu Nairobi ni kubwa na inahitaji kiongozi, Niko tayari kuondoa kesi ni matamshi yake sonko huku akichukua mapumziko kutoka kwa siasa
Gavana wa Nairobi Mike Sonko
Gavana wa Nairobi Mike Sonko Gavana wa Nairobi Mike Sonko

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko akizungumza siku ya JUmamosi akiwa katika kaunti ya Makueni alitangaza kuchukua mapumziko ya miaka 10 kutoka kwa siasa huku akitaka kutupilia mbali kesi yake.

"Watu wanasema wakati wa Mungu ndio bora, nitachukua mapumiko ya mika 10 kutoka kwa siasa, ata vile Uhuru Kenyatta alianguka mwaka wa 2003 alingoja hadi 2013

Nairobi ni kubwa kuliko mtu yeyote." Alisema Sonko.

Mwansiasa huyo alisema kwamba yuko tayari kutupilia kesi yake mbali na kukubali uchaguzi uendelee.

"Kwa sababu Nairobi ni kubwa na inahitaji kiongozi, Niko tayari kuondoa kesi kwa watu kuchagua Gavana wao watakao mchagua." Sonko Alizungumza.

Sonko alidai kwamba Mwenda hakuchaguliwa na wananchi ndio maana wanataka uchaguzi mpya.

"Ni lazima kwa wakaazi wa Nairobi kupata Gavana wanayemtaka Sio kuleta mtu aliyechaguliwa kwa njia  ambayo sio halali.

Wanahitaji kwenda kwa uchaguzi mdogo na kumchagua mtu ambaye wanampenda kupitia kura." Alisema.