'Jina la Mungu litukuzwe milele,'Ruto asema baada ya mahakama kupuzilia mbali machakato wa BBI

Muhtasari
  • DP Ruto azungumza baada ya mahakama kubatilisha mchakato wa BBI
Naibu rais William Ruto akizungumza katika kanisa la House of Hope mtaani Kayole siku ya Jumapili, Januari 10, 2021.
William Ruto Naibu rais William Ruto akizungumza katika kanisa la House of Hope mtaani Kayole siku ya Jumapili, Januari 10, 2021.
Image: DPPS

Naibu Ruto aonekana mwenye furaha baada ya mahakama kubatilisha mchakato wa BBI, haya yanadhibitishwa kupitia ujumbe wake kwenye ukurasa wake wa twitter huku akimshukuru Mungu.

Jibu la DP lijiri dakika chache baada ya benchi la majaji watano wa korti ya katiba Alhamisi kuamuru kwamba mchakato wa BBIni batili.

Majaji Joel Ngugi, George Odunga, Jairus Ngaah, Chacha Mwita, na Teresia Matheka waliamua kwa kauli moja kwamba mchakato mzima ambao timu ya BBI ilifuata kuleta marekebisho ya katiba haukuwa wa katiba.

 

Majaji walisema kuwa rais, serikali, au chombo chochote cha serikali hakiwezi kuanzisha mpango maarufu katika katiba.

Walisema kwamba Muswada wa Marekebisho ya Katiba ya Kenya 2020 ulikuwa mchakato ambao ulianzishwa na rais.

DP Ruto aliwekwa pembeni katika mchakato wa BBI na washirika wake katika Bunge la Kitaifa na Seneti walipiga kura dhidi ya muswada huo.

Majaji walibaini kuwa muswada wa marekebisho ya katiba unataka kupunguza kifungu cha 87 cha katiba na kwa hivyo ni kinyume cha sheria.

Walisema muswada wa marekebisho kuwa ni kinyume cha katiba.

Baada ya auamuzi huo DP aliandika ujumbe ufuatao;

"Kuna MUNGU mbinguni anayependa kenya bila kipimo. Jina la MUNGU lisifiwe milele."