CHANJO YA COVID 19

Kagwe awaagiza ambao hawajapata dozi ya pili kutulia

"Uko heri kwa kupata dozi moja ya chanjo ya AstraZeneca kuliko kukosa. Hatujaskia yeyote aliyeaga kwa kutopata dozi ya pili" Waziri Kagwe asema

Muhtasari

•Waziri Kagwe amewaagiza ambao hawajapata dozi ya pili ya AstraZeneca kuwa  katika hali ya utulivu

•Asema kuwa serikali inatarajia dozi zingine 150000 kutoka nchi za karibu kama DRC

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe ameagiza watu ambao bado hawajapokea dozi ya pili ya chanjo ya AstraZeneca kuwa na utulivu na subira huku akiwaahidi kuwa wataipokea chanjo hiyo.

Ili kuwatuliza, Kagwe amesema kuwa hakuna yeyote aliyedaiwa kuaga kwa kutopata dozi ya pili ya chanjo ya AstraZeneca.

Ushahidi umeonyesha kuwa kupata dozi moja ya chanjo kunakupa ulinzi dhidi ya Covid19  na uko salama kumshinda ambaye hajapata hata dozi moja” Kagwe alieleza.

Akiwa kwenye mahojiano na Larry Madowo siku ya Alhamisi, Kagwe alikiri kuwa chanjo ambazo serikali ilikuwa imeagiza kwa mara ya kwanza ziko karibu kuisha huku zikiwa zimebaki dozi laki moja pekee kutoka kwa dozi milioni 1.12 zilizokuwa zimeagizwa mwezi Mechi.

Serikali inatarajia dozi zingine 150000 kutoka nchi za karibu kama DRC ambako hawana uwezo wa kupeana chanjo hizo kabla ya kuharibika kwake mwezi Juni” Kagwe alisema.

Kufikia siku ya Alhamisi, watu948,980 wamepokea chanjoikiwemo wakongwe, walimu, maafisa wa usalama, maafisa wa afya na wanasiasa.

Waziri huyo amedai kuwa serikali inashiriki mazungumzo na watengenezaji wa chanjo zingine kama Johnson kwani huenda Astrazeneca ikaacha kuwa chanjo ya kipekee Afrika kutokana na kucheleshwa kwa mizigo toka India.