Wakenya 8 wafungwa gerezani Rwanda kwa kosa la wizi wa kimitandao unaohusisha mamilioni ya pesa

Walipatikana wakijaribu kufungua mitandao ya benki ya Equity ile kuiba pesa ya wateja.

Muhtasari

•Wakenya waliokamatwa ni pamoja na Dedan Muchoki Muriuki, Samuel Wachira Nyuguto, Kinyua Erickson Macharia, Godfrey Gachiri Githinji, Eric Dickson Njagi, Rueben Kirogothi Mwangi, Damaris Njeri Kamau na Steve Maina Wambugu.

•Washukiwa wote 12 walipatikana  na hatia ya utundu, kupata habari za kimitandao na lengo ya kutekeleza uhalifu , kubadilisha mitambo ya kompyuta, utumizi wa mitandao bila idhini na wizi.

court
court

Habari na Cyrus Ombati

Washukiwa 12 ikiwemo Wakenya 8, raia wa Rwanda 3 na mmoja kutoka Uganda walipatiwa kifungo cha miaka 8 gerezani na mahakama ya Rwanda kufuatia mashtaka ya uhalifu wa kimitandao 

Kikundi hicho kilikuwa kimetiwa mbaroni mnamo Oktoba 2019 na idara ya kutekeleza uchunguzi nchini Rwanda(RIB) walipopatikana wakijaribu kufungua mitandao ya benki ya Equity ile kuiba pesa ya wateja.

Wanaume saba na mwanamke mmoja kutoka Kenya walikamatwa.

Wakenya waliokamatwa ni pamoja na Dedan Muchoki Muriuki, Samuel Wachira Nyuguto, Kinyua Erickson Macharia, Godfrey Gachiri Githinji, Eric Dickson Njagi, Rueben Kirogothi Mwangi, Damaris Njeri Kamau na Steve Maina Wambugu.

Washukiwa wote 12 walipatikana  na hatia ya utundu, kupata habari za kimitandao na lengo ya kutekeleza uhalifu , kubadilisha mitambo ya kompyuta, utumizi wa mitandao bila idhini na wizi.

Waliagizwa kurejesha shilingi milioni sita za Kenya ambazo benki ilipoteza kufuatia uhalifu huo.

Kesi hiyo ilikuwa imecheleweshwa kufuatia mikakati iliyowekwa kudhibiti ugonjwa wa Corona.

Maafisa ambao walikuwa wanajua kuhusiana na kesi hiyo walisema kuwa Wakenya wale wanane walikuwa wakifuatiliwa sana  kuhusiana na uhalifu wa kimitandao unaohusisha mamilioni ya pesa.

Kirongothi alikaidi dhamana aliyoagizwa kulipa na mahakama ya Kenya kufuatia kesi ya wizi wa kimitandao ambayo alikuwa ameshtakiwa nayo.  Alikuwa ameripotiwa kuiba shilingi milioni 80 kutoka benki moja nchini Kenya kwa kutumia mitandao.

Njagi alikuwa ameshtakiwa na kosa la kuiba shilingi milioni 2.7 kutoka benki moja ya Kenya kwa kutumia mitandao.

Gachiri ambaye alikuwa mfanyakazi katika kampuni ya Standard Group alikuwa ameshtakiwa na kosa la kuiba shilingi milioni 21.5 kutoka kwa benki ya Sidian na K-Rep kwa njia ya wizi wa kimitandao ingawa kesi hiyo ilitupiliwa mbali baada ya pesa hizo kupatikana.