Reuben Kigame atangaza azma ya kuwania Urais 2022 licha ya madai kuwa polisi walikuwa wamemzuia

Kigame alitangaza hadharani azma yake kuwania kiti hicho siku ya Jumatano kupitia video ya moja kwa moja kwenye mtandao wa Facebook.

Muhtasari

•Kigame alichagua kutangaza azma yake jana, Julai 7 kwa kuwa ilikuwa siku ya kuadhimisha miaka 31 tangu  ukombozi wa pili nchini Kenya.

•Kigame pia alikosoa serikali ya sasa inayoongozwa na rais Uhuru Kenyatta na kudai kuwa imekumbwa na wizi mkubwa na madeni

Image: REUBEN KIGAME

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Reuben Kigame ameongeza jina lake kwa orodha ya wagombeaji wa kiti cha urais mwaka wa 2022

Kigame alitangaza hadharani azma yake kuwania kiti hicho siku ya Jumatano kupitia video ya moja kwa moja kwenye mtandao wa Facebook.

Ujumbe wa Kigame kwa wafuasi wake ni 'Rebuild Kenya'(Jenga Kenya upya)

Awali siku hiyo, Kigame alikuwa ametangaza kuwa polisi walimzuia kufanya mkutano wa kuzindua azma yake. 

Licha ya hayo, mwanamuziki huyo mzaliwa wa kaunti ya Vihiga alijumuika na baadhi ya wafuasi wake  na kutangaza kuwa atakuwa kwenye kinyang'anyiro hicho kupitia video aliyopakia kwenye mtandao wa Facebook.

Kigame alichagua kutangaza azma yake jana, Julai 7 kwa kuwa ilikuwa siku ya kuadhimisha miaka 31 tangu  ukombozi wa pili nchini Kenya.

Akitangaza azma yake, Kigame alisuta sana uongozi wa aliyekuwa rais kwa wakati huo, Daniel Arap Moi.

Kigame pia alikosoa serikali ya sasa inayoongozwa na rais Uhuru Kenyatta na kudai kuwa imekumbwa na wizi mkubwa na madeni.

Mwanamuziki huyo ambaye alipata umaarufu mkubwa kutAliapa kuwa ataunganisha Kenya iwapo atachaguliwa kuwa rais.

"Nitaunganisha Wakenya wawe ni jamii moja na kumaliza maombo ya ukabila. Mwenyewe nilizaliwa magharibi mwa Kenya, nikasomea Kisumu na Thika, nikamua mke mkikuyu, ninaishi Uasin Gishu. Sasa mimi ni Mluhya, Mjaluo, Mkikuyu ama Mkalenjin? Si mimi ni Mkenya?" Alisema Kigame.

#lipotumaini #rebuildkenya #kigameforpresident

Posted by Reuben Kigame on Wednesday, July 7, 2021

Ujumbe wa Kigame kwa wafuasi wake ni 'Rebuild Kenya' (Jenga Kenya upya)

Kigame atamenyana na wengine ambao washatangaza azma yao kama naibu rais William Ruto, Musalia Mudavadi, Kalonzo Musyoka, Alfred Mutua, Mukhisa Kituyi kati ya wengine.

Alisihi Wakenya kuunga mkono kampeni yake kwa kumchangia msaada wa fedha.