•Makomere Shikokongo (35) , John Omoro (25) na Joseph Amakobe (40) walikuwa wanapimana nguvu nje ya nyumba ya mama yao katika kijiji cha Ibokolo, kaunti ya Kakamega kuhusiana na mzozo usiojulikana wakati msiba huo ulitokea.
Vita kati ya ndugu watatu iligeuka kuwa mauti baada ya mmoja wao kumgonga mama yao vibaya alipojaribu kuwatenganisha na kumsababishia maumivu yaliyomwangamiza
Wakati vita kati yao ilikuwa imechacha, mama yao aliingilia kati akikusudia kuwatenganisha ila mmoja wao , ambaye alitaka kitanzi kiendelee kutamba akamgonga na kumwangusha chini.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 60 alianza kulalamika kuhusu maumivu mabaya mwilini ila hakuna aliyempeleka hospitali. Baaadae alipatikana akiwa amefariki ndani ya nyumba yake.
Kufuatia hayo wapelelezi walimtia mbaroni mshukiwa mkuu, Makomere Shikokongo ambaye anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.