Watoto wa Mitaani wabadilisha Mbwa kitoweo-Molo

Muhtasari

•Wakaazi hao wa Molo wameiomba serikali kubuni mpango utakaosaidia wavulana wa mitaani kupata chakula na malazi.

•Baadhi ya sababu ya watoto hawa kujiingiza kwenye vitendo hivyo ni kutokana na ukosefu wa kazi, na njaa ambayo imeikumba nchi.

Mbwa waliofungiwa kwa ajili ya kuchinjwa huko Korea
Mbwa waliofungiwa kwa ajili ya kuchinjwa huko Korea
Image: COEXISTENCE OF ANIMAL RIGHTS ON EARTH (CARE)

Watoto wa mitaani huko Molo wamechinja Mbwa na kuibadilisha kuwa kitoweo,tukio hilo ilidhibitishwa na mkaaji  wa Molo Simon Munene akizungumza na wanahabari.

''Niliona moshi kutoka kwenye nyumba,nikadhani  kuwa inaungua,kufika ndani nikakuta nyama sakafuni kiko tayari  kupikwa'' Simon alisema.

Wavulana hao walisema kuwa  walihisi njaa na hii iliwalazimu kuchinja mbwa iliwapate kitu cha kukula.

Wakaazi hao wa Molo wameiomba serikali kubuni mpango utakaosaidia wavulana wa mitaani kupata chakula na malazi.

''Najua maisha ni magumu, lakini hapa Molo hatujafikia kiwango hicho cha kula mbwa, hawa watoto wa mitaani wanateseka kwa kweli'' Simon alisema.

Wakaazi wa Molo pia wamekubali kukuja na mpango ambao utawasaidia watoto wa mitaani kupata vyakula na malazi.

Mchango mdogo kutoka kwa wakaazi hao ili kutimiza ndoto hii ni kitu ambacho kimeungwa mkono na watu wengi.

''Ninajua ya kwamba wale ambao watafikiwa na jambo hili,tushirikiane pamoja ili kusaidia hawa watoto,kama uko na Viazi, chochote kile wewe leta''Simon alisema.

Aliongeza kwa kusema kuwa Chifu, Mwakilishi Wadi na Mbunge  wa eneo hilo wajitokeze wote kuwasaidia watoto hawa,kuna wengine wanahitaji kupelekwa Hospitalini.

''Mpango huu utasaidia hawa watoto kwa kupata mahitaji ya msingi katika maisha ya mwanadamu'' aliongezea.

Baadhi ya sababu ya watoto hawa kujiingiza kwenye vitendo hizo ni kutokana na ukosefu wa kazi, na njaa ambayo imekumba nchi.

Pia iliripotiwa kuwa watoto hao hawajawahi kulazwa hospitalini kwa shida yoyote inayotokana na kukula  Mbwa,Paka, Panya na Punda kwa zaidi ya miaka miwili.

''Punda anapogongwa na gari wanalikusanya kisha wanalipika, jambo la kusikitisha ni kwamba, wakikutwa na Polisi wakiwa wamelala nje , wanakamatwa na kupelekwa selI badala ya serikali kuwasaidia  kupata kazi na chakula'' John alisema.