Ndege ya kijeshi yaanguka kwa kishindo na kuteketea Kajiado

KDF imethibitisha kuwa ndege hiyo ilikuwa ndege ya kijeshi aina ya Mi 171e ambayo ilikuwa katika harakati za mazoezi.

Muhtasari

•Kamanda wa polisi upande wa Kajiado, Muthuri Mwongera amesema kuwa ajali hiyo ilifanyika mida ya saa mbili asubuhi siku ya Alhamisi. Hata hivyo, amesema kuwa idadi ya abiria waliokuwa ndani bado haiathibitishwa.

Eneo la tukio
Eneo la tukio
Image: Hisani

Ndege moja aina ya chopper imeanguka katika maeneo ya Oltinga, Kajiado likiwa limebeba idadi isiyojulikana ya  abiria.

Kamanda wa polisi upande wa Kajiado, Muthuri Mwongera amesema kuwa ajali hiyo ilifanyika mida ya saa mbili asubuhi siku ya Alhamisi. Hata hivyo, amesema kuwa idadi ya abiria waliokuwa ndani bado haiathibitishwa.

"Nimetuma OCPD wa Kajiado Magharibi, Vincent Kitili kutujulisha hali ilivyo pale" Mwongera alisema.

Mwongera amethibisha kuwa ndege hiyo ambayo ni ya jeshi ilianguka kilomita 60 kutoka Oloopolos.

Ndege kama zile husemekana kubeba abiria 26.

OCPD wa Kajiado Magharibi , Vincent Kitili amesema kuwa abiria 13 walinusuriwa na kupelekwa hadi hospital ya Forces Memorial, Nairobi.

"Hii ni operesheni ya kijeshi na hatufai kutoa habari zozote kuhusiana na yanayojiri kwenye eneo la tukio. Jeshi limechukua majukumu hayo. Jukumu letu ni kuandika ripoti baadae." Kitili alisema.

Mkuu wa wilaya, Morekwa Morang'a amesema kuwa ndege hiyo lilikuwa inajiandaa kutua wakati upepo ulitokea na kumfanya rubani asiweze kuona chini.

"Bado hatujahesabu mili tujue wangapi walipoteza maisha yao" Morang'a alisema.

Alisema kuwa ndege ile ilikuwa katika harakati zake za kawaida wakati ajali hiyo ilitendeka baada ya kupaa kutoka uwanja mdogo wa ndege wa Eastleigh asubuhi ya Alhamisi.

Mashahidi wamesema kuwa ndege hiyo ililipuka na kuteketea punde baada ya kuanguka.

KDF imethibitisha kuwa ndege hiyo ilikuwa ndege ya kijeshi aina ya  Mi 171e  ambayo ilikuwa katika kazi ya mazoezi.

"Ilianguka na kulipuka katika maeneo ya Ol Tepesi, Kajiado" KDF iliandika kwenye mtandao wa Twitter.

.

.

.

(Mengine yatafuata)

(Mtafsiri: Samuel Maina)