Baba ya Mbunge wa Dagoretti Kusini John Kiarie afariki

Mbunge huyo ambaye anahudumu kwa muhula wake wa pili bungeni alitangaza kufariki kwa baba yake kwenye mtandao wake wa Twitter.

Muhtasari

• Ng'ethe ambaye kwa wakati mmoja alihudumu kama mbunge wa Kandara amefariki baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu. 

• David Waweru Ng'ethe, aliwahi kuwania kiti cha urais mara tatu bila mafanikio.

Baba yake John Kiarie aliyekuwa mbunge wa Kandara David Ng'ethe.
Baba yake John Kiarie aliyekuwa mbunge wa Kandara David Ng'ethe.
Image: JOHN KIARIE

Babake mbunge wa Dagoreti Kusini John Kiarie, David Ng'ethe  ameaga dunia.

Ng'ethe ambaye kwa wakati mmoja alihudumu kama mbunge wa Kandara amefariki baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu, mwanawe, John Kiarie amesema. 

“Simba imepumzika.Saa ya giza .Wakati jua la saa 3 alasiri lilipopambana na wingu jeusi, kwa ajili ya ukuu angani, saratani kaidi ilipiga pigo la mwisho. Hakika kifo ni hatima, haiaminiki.” Aliandika Kiarie katika mtandao wake wa Twitter.

David Waweru Ng'ethe, aliwahi kuwania kiti cha urais mara tatu bila mafanikio.

Ng'ethe alijiunga na siasa 1981 baada ya mahakama kubatilisha ushindi wa marehemu George Ndung'u Mwicigi.

Alihudumu hadi mwaka wa 1983 alipotimuliwa na mpinzani wake wa kisiasa Mwicigi.

Mwanasiasa huyo alikuwa mbunge wa nne wa Kandara tangu ilipoanzishwa mwaka wa 1963.

Meza ya Radio Jambo yatuma risala za rambi  rambi kwa familia ya marehemu Ng'ethe wakati huu mgumu.