Mtoto aliyeng'olewa macho Kisii aambia makama kuwa nyanyake ndiye alitenda unyama huo

Sagini alisema alitumwa kuchota maji na akiwa njiani alivamiwa na mshukiwa aliyemng'oa macho.

Muhtasari

• Wakati wa kuhojiwa mtoto Sagini alisema mshtakiwa aliondoa macho yake kwa mikono kabla ya kupelekwa katika shamba la mahindi ambapo alipatikana ametupwa. 

Washukiwa wa kisa cha kumng'oa macho mtoto Sagini wakiwa kizimbani
Washukiwa wa kisa cha kumng'oa macho mtoto Sagini wakiwa kizimbani
Image: MAGATI OBEBO

Mtoto Brighton Junior Sagini siku ya Ijumaa alieleza mahakama hatua kwa hatua matukio kabla ya kung’olewa macho na kumhusisha nyanyake Rael Nyakerario, 84 na tukio hilo ambalo limemuacha mtoto huyo bila macho.  

Katika video iliyorekodiwa, mtoto huyo kupitia kwa mtaalamu wa watoto aliambia mahakama kuwa nyanyake alipanga kung'oa macho yake kabla ya kumtupa katika shamba la mahindi lililo karibu. 

Nyakerario ni miongoni mwa washukiwa wengine, Alex Ochogo na Pacificah Nyakerario wanaokabiliwa na mashtaka ya kumtesa na kumjeruhi mtoto Sagini katika mahakama ya Kisii. 

Washukiwa walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Christine Ogweno siku ya Ijumaa.  Wakati wa kuhojiwa Ijumaa mtoto Sagini alisema mshtakiwa aliondoa macho yake kwa mikono kabla ya kupelekwa katika shamba la mahindi ambapo alipatikana ametupwa. 

Siku hiyo, Sagini alisema alitumwa kuchota maji na akiwa njiani alivamiwa na mshukiwa aliyemng'oa macho. Alikimbizwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Kisii baada ya matibabu ya dharura katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Marani. 

Daniel Nyameino, Daktari wa Kliniki katika kituo hicho alisema alikuta macho ya Sagini yakivuja alipoletwa hospitalini. Mtoto huyo alikuwa na alama za mikwaruzo kwenye jicho lake la kulia ikiashiria dalili za kudulumiwa na mvamizi akitoboa macho yake. 

Nyameino aliambia mahakama kuwa majeraha hayo yalitokana na kifa chenye ncha kali. Kesi hiyo itaendelea Machi 17 na kusikilizwa kwa mara ya mwisho Machi 24.

 

TAFSIRI: DAVIS OJIAMBO