Vita vya mapenzi

Kibiriti ngoma awakosanisha mtu na babake

Rebbeca hajaonekana tangia hapo na wengi wanasema amezihamishia huduma zake hadi mjini Eldoret .

Muhtasari
  • Kesho yake ,akitaka kujua  iwapo ni ukweli kwamba mpenzi wake alikuwa pia akionana na babake ,jamaa huyo aliamua kwenda naye katika hoteli ile ile ili kuona iwapo kuna wahudumu watakaomjua .
  • Vita hivyo vilivyodumu saa kadhaa huku kila mmoja kati ya baba na mtoto wake akitumi chochote alichopata mbele kumpigia mwenzake .Polisi ndio walioingia kati kuwaeka seli hadi kesho yake

 

kahaba
kahaba

 

Kahaba mmoja mrembo amewafanya mtu na babake kuzabana makofi na kurushiana  makonde mazito mazito  katika danguro moja  vungani mwa ji wa Turbo.

Chanzo cha vita vyao ni kwamba kila mmoja kati yao anadaiwa kwamba mwanamke huyo ni mpenzi wake lakini wakaazi wanafahamu kwamba licha ya ‘kuwacheza’ kwa kuchuma kutoka  nyungu zao wawili , mwanamke huyo pia ni  kahaba  na anafahamika sana kwa kutoka na wanaume wengi wanaofanya kazi za kuendesha matrela ya masafa marefu . Amewateka fikra  mtu na babake kwa kiasi kwamba hakuna kati yao anayeamini kwamba mwanamke huyo huuza mwili wake ili kupewa pesa .

Masaibu yaliyopeleka vita kuzuka kati ya mtu na mwanawe yalianza siku ambayo rais Uhuru Kenyatta alitangaza kwamba muda wa kafyu sasa utazidishwa ili kuanza kutekelezwa saa tatu za usiku na sio  saa moja . Hatua hiyo iliwafanya watu wengi kzuidisha shughuli zao hadi nyakati za usiku  pasi na kuogopa viboko vya polisi ambavyo  wengi walikuwa wanaogopa kuanzia saa moja . Siku huyo mwanamke huyo aliyetambuliwa kama Rebbeca alikuwa katika mkahawa mmoja na  mwanamme ambaye wengi walijua kwamba Rebbeca alikuwa apia’akimhudumia’ babake katika eneo hilo .

Kesho yake ,akitaka kujua  iwapo ni ukweli kwamba mpenzi wake alikuwa pia akionana na babake ,jamaa huyo aliamua kwenda naye katika hoteli ile ile ili kuona iwapo kuna wahudumu watakaomjua . kwa bahati mbaya ,mmoja wa wahudumu hao  alipasua mbarika alipomuuliza yule mwanadada iwapo ni yeye alikuwepo pale ba ‘babake’ siku iliyotangulia . Hapo ndipo ndipo  sarakasi zilipoanza , jamaa alianza kufoka akimshtumu babake kwa kutaka kuharibu uhusiano wae na Rebbeca na kwenda katika  hadware ya mzee wake ili kumkabili kwa lengo la kumkomesha .  mji wote ulisimama  kushuhudia baba na mwanawe wakimpigania mwanamke Yule ambaye hakuna aliyekosa kumjua kwamba alikuwa kahaba katika sehemu hiyo .

Vita hivyo vilivyodumu saa kadhaa huku kila mmoja kati ya baba na mtoto wake akitumi chochote alichopata mbele kumpigia mwenzake .Polisi ndio walioingia kati kuwaeka seli hadi kesho yake .Rebbeca hajaonekana tangia hapo na wengi wanasema amezihamishia huduma zake hadi mjini Eldoret .