Valentine's

Valentine's iko hapa! Jinsi unavyoweza kuadhimisha siku hiyo ya wapendanao

Siku ya valentine , toa bonge la tishio kwa kuvalia kichapo swafi ambacho hata mwenzio kitampa tabasamu .

Muhtasari
  • Unaweza kuamua kutulia tu nyumbani mkinong’onezeana  na mwenzio . 
  • Unachofanya siku hii kisiwe kitu ambacho umekifanya muda wote kila siku bali piga shughuli zako kitofauti ili kuzua kumbukumbu

Tarehe 14 Februari huwa siku  bomba sana kwa wapendanao yaani valentine .Kila siku inafaa kuwa ya mapenzi lakini siku hii ,ni spesheli kwa wapendanao na iwapo umekuwa ukijisumbua fikra kuhusu unachoweza kufanya tofauti mwaka huu basi hapa nimekuandaliwa mwongozo  tosha wa mambo unayoweza kuyafanya ili kumteka kimahaba mwenzako .

 Jitulize chumbani ,sitisha shughuli za kawaida umpe muda wako.

  Siku ya valentine ,hakikisha angalau unampa mwenzako muda wako .Haitakuwa spesheli iwapo shughuli zako na ratba zitasalia kama siku nyingine . Unaweza kuamua kutulia tu nyumbani mkinong’onezeana  na mwenzio .  Unachofanya siku hii kisiwe kitu ambacho umekifanya muda wote kila siku bali piga shughuli zako kitofauti ili kuzua kumbukumbu

Mjulie Hali mwenzio,mshtukize kwa ujumbe wa kuvutia

  Siku  hii iwapo utakuwa mbali na mwenzio ,hakikisha angalau anapata ujumbe wako ili afahamu kwamba  unamfikiria na unamjali uliko . Baadhi ya watu hupuuza kutumiana jumbe lakini  sms moja tu ya kumjulia mwenzako hali siku inapoanza au kumalizika inaweza kuyeyusha  theluthi ya makovu na kuifanya barafu laini ya penzi

 

Mvalie kipya ambacho kitamnata,muache kinywa wazi

   Siku ya valentine , toa bonge la tishio kwa kuvalia kichapo swafi ambacho hata mwenzio kitampa tabasamu .  Mavazi yako ya kazini au nyumbani na yaliochanika au aliyoyazoea yaweke kando . Muangamize kwa mvuto  wako mpya na mg’aro mzuri wa kwatuo lako siku hii .

Jali kuhusu anachofikiria ,pata maoni yake katika angalau jambo linalowahusu nyote .

  Zungumza na mwenzio kuhusu nyinyi tu.Huu sio wakati wa kujadiliana kuhusu jinsi ya kulipa mkopo wenu au ugumu wa kazi au mwezi unavyojikokota.Huu ndio wakati tosha wa kutoa matokeo na tathmini ya uhusiano wenu .Jua mwenzako  anataka nini na yuataka vipi .

Mshirikishe katika kitu au mchezo usio  katika ratiba yenu ya kawaida.

  Fanyeni mchezo wenu pekee ambao utawafanya  kujipata katika mandhari ya kitoto . jichekesheni kwa njia ya kipekee  na msiogope kuonekana  mkifanya mchezo wowote unaowarejesha utotoni .

Mueleze kuhusu hofu zako na matarajio,mfanye awe msiri wako wa kwanza.

  Mpenzi wako ndiye anayekufaa kupa jeki kimawazo na panapo jambo ambalo huwezi kumwambia yeyote ,basi fanya hima ya kumpa muda ili akufahamishe kuhusu yote anayoazimia,kuhofia na hata kumueleza siri ambazo kwa kawaida huwei hata kuzitoa.Offcourse,usije kutaboa siri  ambazo zitavuruga siku nzima ya Valentine kasha ukanilaumu.

 Jilegeze machoni pa mwenzio,usijibanie katika urasmi .

  Siku hii ,sio ya kujipa urasmi na ukawaida wa kila siku . jiachilie kama wanavyosema wasasa.ingawa kuwa mwangalifu usijivuruge kabisa ukakosa ustaarabu .Hii inaeleweka sana kwa urahisi iwapo kumekuwa na tofauti kidogo na mwenzio,jaribu kumpa tulizo angalau ili umpe fursa ya kujieleza na kujitetea .