Mahusiano

Je , pengo la umri ni kitu kikubwa katika uhusiano?

Utafiti uliofanywa na jarida la Allure umeonyesha kwamba wanawake huwa warembo Zaidi wakiwa na umri wa miaka 30

Muhtasari
  • Sasa kumekuwa na mjadla kuhusu umri katika mapenzi na iwapo mapenzi yanayohusisha mwanamke mwenye umri wa juu kumliko mwanamme hufaulu
  • Mifano ni mingi ya waliopendana ,kufunga pingu za maisha na hataa kuishi hadi sasa na wenzao licha ya wanawake kuwa na umri  Zaidi ya wanaume
Msanii Guardian Angel na mpenzi wake Esther Musila

Mapenzi ni kikohozi hayawezi kufichika –unasema msemo wa zamani ambao wakati mwingi umetubwaga kwani wengi ambao hawakutarajiwa kuwa katika mahusiano ya mapenzi walipendana na kuishi maisha yao bila  nyongo .

Sasa kumekuwa na mjadla kuhusu umri katika mapenzi na iwapo mapenzi yanayohusisha mwanamke mwenye umri wa juu kumliko mwanamme hufaulu . Kulingana na utafiti wa kijamii ,umri hauna athari yotote kwa mapenzi ili mradi wanaopendana wafahamu kwamba mapenzi yao hayategemei tofauti ya umri wao .

Mifano ni mingi ya waliopendana ,kufunga pingu za maisha na hataa kuishi hadi sasa na wenzao licha ya wanawake kuwa na umri  Zaidi ya wanaume . Utafiti uliofanywa na  jarida la  Allure umeonyesha kwamba  wanawake huwa warembo Zaidi wakiwa na umri wa miaka 30 ,huonyesha daalili za kuzeeka wakiwa na umri wa miaka 41 na  hukoma kuwa ‘sexy’ wakiwa na umri wa miaka 53 ilhali hutajwa kama wazee wakiwa na umri wa miaka 55 .

Kwa upande wao ,wanaume  walipatikana kuwa watanashati wakiwa na umrio wa miaka 34  ,huanza kuzeeka wakiwa na umri wa miaka 41  hukoma kuonekana kama wanaovutia wakiwa na umri wa miaka 58 na hutajwa kama wazee wanapogonga umri wa miaka 59 .

Wa hivi punde kutukumbusha kwamba mapenzi hayana mipaka ya umri ni msanii wa gospel  Guardian Angel  ambaye amejipata kamezwa katika lindi la mapenzi  na mwanamke mwenye umri wa miaka 50 Esther Musila  ambaye ana watoto watatu wenye umri wa miaka   29,26 na 22. Hilo halijawazuia yeye na Guardian Angel kujivinjari na kupata kila raha ya penzi lao kwani Msanii huyo yupo katika miaka ya 20 . Guadian Angel ambaye pia kama  Esther anapenda sana kufanya mazoezi na kuna mengi yanayowaleta pamoja kuliko hilo kwani kando na ujasiri wa kuweka wazi uhusiano wao ,wawili hao wanaonekana kufaana kwa kila hali .

Kwa mujibu wa tafiti nyingi kuhusu suala hilo la mwanamke kumzidi mume wake umri ,wataalam wanasema hapafai kuwa na tatizo isipokuwa kuna athari za ‘nje’ ambazo huvuruga mahusiano kama hayo .Wakati mwingi ,shinikizo hutokea kwa marafiki au jamaa za mwanamme ambao huchukulia uhusiano kama huo kama wa muda na hivyo basi kuwavuruga wapendanao ambapo wasipokuwa na ujasiri ,wengi hujipata wamevunja  mapenzi yao kwa ajili ya mambo yanaofanywa au kusemwa na watu walio karibu nao . Afrika ina matatizo hasa kuhusia na ndoa  ama mahusiano kama hayo kwa sababu kuna  mtindo wa wanaume kuwaoa wasichana wa umri mdogo ingawaje katika mataifa yaliyoendelea ,suala la pengo la umri kati ya mwanamke na mwanamme halijawahi kuchukuliwa kama kubwa .