Wafahamu wahubiri waliotumia nyoka, petroli, dawa za kuuwa wadudu 'kutenda miujiza'

chunguzi uliofanywa na stesheni ya runinga ya KTN nchini Kenya , Novemba 2014 ulifichua mbinu alizotumia Victor Kanyari, mchungaji maarufu ambaye alidaiwa kuwadanya waumini katika katisa lake la Salvation Healing Ministry.

Muhtasari

•Alikuwa anatumia kemikali ambayo inabadilika kwa haraka kwenye maji na kuwa nyekundu, kuwaoshea miguu waumini wake na kudai kuwa damu inatoka miguuni na hiyo ni saini ya kupona.

•Askofu Daniel Obinim wa kanisa la International Godsway nchini Ghana aliwahi kusimama juu ya tumbo la mwanamke ambaye aliripotiwa kuwa mjamzito, akidai kuwa anamuombea kumtoa mashetani.

mhubiri akiweka nyoka kwa mdomo wa muumini
Hisani mhubiri akiweka nyoka kwa mdomo wa muumini

Ufichuzi kwamba muhubiri mmoja wa Afrika Kusini alikuwa akiwapulizia dawa ya wadudu waumini wa kanisa lake uliwashangaza wengi, lakini hakuwa muhubiri wa pekee barani Afrika kutekeleza vitendo kama hivyo vinavyowacha maswali mengi.

Miji mikuu na ile midogo barani Afrika imejaa mabango na matangazo tofauti yanayokuza makanisa yakiwa na vivutio vya kuponya mara moja na kuwaokoa watu walio katika hali mbaya au maradhi.

Makanisa hayo kawaida huongozwa na wahubiri wenye haiba , ambao walianza wenyewe nyumba hizo za Mungu badala ya kujiunga na makanisa imara na mara nyingi hudai kuwa na uwezo wa miujiza.

Hatahivyo, miujiza hiyo ndio inayowavutia waumini kwa mfano 'kupanda mbegu', ama kutoa fedha kwa wahubiri hao.

Hawa ni baadhi ya wahubiri wa Afrika waliozua utata:

'Kubadilisha Mafuta ya petrol hadi kuwa juisi ya mananasi'

mhubiri akishikilia chupa ya mafuta ya petrolii
mhubiri akishikilia chupa ya mafuta ya petrolii
Image: Hisia

Pastor Lesego Daniel anaongoza kanisa la Rabboni lililopo katika mji wa Afrika Kusini wa Pretoria.

Alisifika kwa kuwaagiza waumini wa kanisa lake kunywa mafuta ya petroli , akidai kwamba ameyabadilisha na kuwa juisi ya mananasi.

Kanda ya video iliosambazwa mtandaoni wakati huo ilionesha muumini mmoja akimwaga petrol hiyo katika kifaa kimoja na kuiwasha moto ili kuthibitisa kwamba ilikuwa inaweza kuwaka.

Baadaye anakunywa na kutangaza kwamba anahisi yuko shwari na kwamba hana madhara yoyote aliopata wakati muhubiri anapouliza kuhusu ladha..

Mwanamke mmoja baadaye anaonekana akikimbilia mbele ya kanisa hilo ili kunywa kinywaji hicho na baadaye kutangaza kwamba ni kinywaji kitamu na cha kuvutia - kitu kilichowavutia wanawake wengine pia kufanya.

"Hatahivyo kiwango cha upako hakiko sawa, Iwapo huwezi kubadilisha maji kuwa mvinyo usijaribu nyumbani.''

'Muhubiri wa nyoka'

Penuel Mnguni amekuwa akiendesha kanisa la End Times Dsiciples tangu 2014.

Yeye amefunzwa uhubiri na Muhubiri Lesego Daniel, Muhubiri wa Afrika kusini ambaye alitumia dawa ya kuuwa wadudu katika uponyaji wake.

Mwaka huohuo alifungua kanisa lake , likiwa na picha za waumini wakila nyasi na maua kutokana na maagizo yake ambapo zilisambazwa katika mtandao wa facebook na tovuti ya kanisa hilo.

Picha nyengine zilionesha muhubiri huyo anayejiita mtume akiwalisha waumini wake mawe ambayo alidai kuyabadilisha kuwa mikate.

Alipatiwa jina la 'Snake Pastor'{muhubiri wa nyoka} baada ya picha kuzuka akiwalisha waumini wake nyoka na panya , ambao alidai wamebadilishwa na kuwa chokoleti.

'Kutibu sehemu za siri

Mhubiri akishika sehemu za siri za muumini
Mhubiri akishika sehemu za siri za muumini
Image: Hsia

Nchini Ghana, Askofu Daniel Obinim wa kanisa la International Godsway ameongeza orodha ya mbinu anazotumia katika maombi au kufanya miujiza.

Katika tukio moja, ambalo lilishirikishwa na wengi , alikuwa amesimama juu ya tumbo la mwanamke ambaye aliripotiwa kuwa mjamzito, alidai kuwa anamuombea kumtoa mashetani.

Tukio lingine lililoshangaza wengi Juni, 2016,alionekana akiwa ameshikilia nguo ya mwanaume katika sehemu zake za siri akimuombea ili sehemu hiyo iweze kufanya kazi vizuri.

Mwanaume akiwa amesimama huku akiwa amenyoosha mikono yake juu , akisubiri mchungaji kushika sehemu zake za siri.

Hii inaonekana kuwa mbinu anayotumia katika maombi yake ili kutibu wanaume wanaosumbuliwa na matatizo ya nguvu za kiume.

Katika video nyingine ambayo ilishirikishwa mtandaoni, alikuwa anamuombea mwanaume ambaye uume wake ulikuwa haujavalishwa nguo.

Alimuadhibu msichana mmoja na mwanaume wakati wa ibada kwa madai kuwa walifanya mapenzi nje ya ndoa.

Mchungaji mmoja alionekana akimshikilia mwanamke aliyekuwa akijaribu kukimbia.

Mchungaji alionekana akimchapa kwa mkanda muumini , huku waumini wakiwa wamekaa.

Taarifa za vyombo vya habari katika mahakama ya mjini Accra zilitaka mchungaji huyo akamatwe na wasaidizi wake kwa madai ya kuwachapa vijana wawili kanisani.

'Damu kwenye maji'

Kanyari akibadilisha maji kuwa mekundu
Kanyari akibadilisha maji kuwa mekundu
Image: Hisia

Uchunguzi uliofanywa na stesheni ya runinga ya KTN nchini Kenya  , Novemba 2014 ulifichua mbinu alizotumia Victor Kanyari, mchungaji maarufu ambaye alidaiwa kuwadanya waumini katika katisa lake la Salvation Healing Ministry.

Alikuwa anatumia kemikali ambayo inabadilika kwa haraka kwenye maji na kuwa nyekundu, kuwaoshea miguu waumini wake na kudai kuwa damu inatoka miguuni na hiyo ni saini ya kupona.

Msaidizi wake mmoja wa zamani alionesha namna ambavyo mchungaji huyo anavyotumia mbinu hiyo.

Video nyingine inamuonesha mchungaji huyo akiweka mkono wake ndani ya gauni ya mwanamke mmoja na kushika matiti yake, huku akisema atapona saratani ya matiti.

Mwanamke alionekana akigeuka kutokutana na kamera lakini mchungaji alikuwa anamlazimisha kugeuza uso ili kuwaangalia waumini ili waone jinsi anavyoshika matiti yake na wote waweze kona.

Na baada ya hapo aliwaita wasaidizi wa kanisa na kuleta mafuta ya uponyaji.

Utafiti ulisema kuwa Kanyari alikuwa mtoto wa Nabii Lucy Nduta, mchungaji mwingine ambaye alikamatwa mwaka 2009 kwa kuwadanganya watu wasio na uwezo kwa madai kuwa anaweza kutibu Ukimwi.

Muda mfupi baadae , alionekana katika kipindi kingine cha luninga , akisema ilikuwa ni kazi ya maadui zake.

Kanyari bado anahubiri mpaka sasa.

(Tahariri na Samuel Maina)