Kwa nini wanawake husalia kwa wenza wao, licha ya vipigo vya kinyama wanavyopata?

Muhtasari

•Janga la corona lilipotangazwa mwaka 2020, mataifa mengi yaliweka vizuizi ili kuzuia maambukizi ya Corona na hali hii ilileta changamoto kwa maisha ya kawaida ya watu

Image: GETTY IMAGES

Janga la corona lilipotangazwa mwaka 2020, mataifa mengi yaliweka vizuizi ili kuzuia maambukizi ya Corona. Hali hii ilileta changamoto kwa maisha ya kawaida ya watu. Biashara zilisambaratika,uchumi ukazorota na mamilioni ya watu wakapoteza ajira duniani.

Familia nyingi zikaanza kuzozana kutokana na ukosefu wa mapato na uwezo wa kukidhi mahitaji ya familia. Wanawake kwa wanaume waliokosa ajira na mzigo wa kulea familia ukasababisha vita baina ya wanandoa. Mizozo hiyo ikasababisha kesi za dhulma za kijinsia kuongezeka duniani.

Familia moja iliyoathirika jijini Nairobi inaashiria changamoto hizi. Mama Elizabeth aliishi jijini humo na mumewe bila shida hadi walipokosa kazi kwa sababu ya janga la Corona lililowafanya kukaa ndani ya nyumba kwa muda, kutokana na marufuku ya kutotoka nje. Muda si Muda,ugomvi wa watoto kukosa chakula ukasababisha maafa.

Mama Elizabeth anaeleza mumewe alichoshwa na maswali ya fedha. Siku moja baada kurudi kutoka kutafuta kazi mume akamshambulia ELizabeth. “Akanipiga ngumi ,akaanza kuniyonga, nikamsukuma nikatoroka nje,akanifuata na akaniangusha chini akanikanyaga. Nilipojaribu kuamka sikuweza,kumbe mguu ulikuwa umevunjika”.

Ukosefu wa pesa na ajira ulisababisha wanawake wengi kuvumilia mateso

Mwathiriwa Elizabeth alikuwa na bahati ya kwamba mamake mzazi alimpokea. Lakini gharama zilimemzidi mamake na akamfukuza Elizabeth. Ilimbidi Elizabeth atafute makao mengine,na hakuwa na budi kurudi nyumba ya mateso aliyoitoroka. Biashara yake ya kuuza nguo ilikuwa imesambaratika kutokana na atahri za corona.

Alisalia kumtegemea mumewe,yuleyule aliyemdhulumu miezi mitatu tangu alipotoroka. Elizabethaliishi kwa uoga na mumewe baada ya kurudi wake anasema “nikilala naficha visu ,nahofia ataleta kelele tena nilikuwa na wasiwasi mkubwa licha ya kwamba nilirudi kwa mume wangu.”

Miezi sita baadaye,Elizabeth na mumewe wakaanza kuzozana tena,kiasi cha kwamba mumewe alimpiga huku akiwa mja mzito. Wakati huu Elizabeth alijinusuru kwa tangazo alilosikia kwenye radio. Elizabeth akakimbilia hifadhi ya wanawake . Nyumba kadhaa zilikuwa zimejaa,ila washauri wa shirika la CrewaKenya walimsaidia kupata nafasi..wakati huu wote ujauzito wake ulikuwa umeanza kutatizika kutokana na kipigo alichopata kutoka kwa mumewe….

Uhaba wa nyumba za kuhifadhi wanawake waliodhulumiwa

Kilio cha elizabeth ni kati ya taarifa nyingi kutoka kwa wanawake ambao ni waathiriwa wa dhulma za kijinsia katika msimu wa Corona. Shirika la CrewaKenya wanasema idadi ya wanawake waliotoaka hifhadhi katika nyumba za wanawake waliodhulumiwa iliongezeka. Nereah Akoth mshauri wa CREWAKENYA nasema “Kwa kawaida wengi wao wangekimbilia kujinusuru katika nyumba za jamaa zao,lakini kutokana na agzo la serekali la kutotangamana,familia nyingi zilikata kuhifadhi dada zao. Familia ambazo hapo awali walitoa hifadhi kwa jamaa zao wakaogopa maambukizo ya virusi vya corona na kufunga milango yao kwa walodhulumiwa.

Mashirika ya serikali; kituo cha utafiti wa uhalifu wa kitaifa na baraza la kitaifa linalosimamia utekelezwaji wa sheria waliripoti kuongezeka kwa visa vya unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana kwa asilimia themanini na saba wakati wa marufuku ya kutotoka nje kwenye msimu wa corona katika mwaka elfu mbili na ishirini.

Image: GETTY IMAGES

Serekali ya Kenya walaumiwa kwa kutotekeleza sera kikamilifu

Kutokana na takwimu hizi,wizara ya jinsia ilielekezewa kidole cha lawama katika kutekelza sera zinazohakikisha usalama wa waathirika na kupatikana kwa haki mahakamani.

Katibu msaidizi wa wizara ya jinsia Rachel Shebesh anasema “ Janga la Corona lilitufungua macho, tuliona uhaba wa hifadhi za wanawake waliodhulumiwa kwani tuko na nyumba kumi na mbili katika kaunti arobaini na saba. Vituo vya polisi vya kukabiliana na kesi za dhulma za kijinsia hazikuwepo na hata hospitalini sehemu maalum ya kushughulikia waathirika pia zilikuwa nadra. Tumebadilisha haya yote,tunaimarisha huduma hizi”.

Utata wa kupata haki

Mwathirika Elizabeth alielezea masaibu yake katika kituo cha polisi. Anasema “Waliniambia niende nipone mguu,ule uliovunjika wakati mume wangu aliponipiga, halafu nikirudiwatanisaidia.Mimi nilikata tamaa nikawachana na hiyo kesi”.

Polisi nchini Kenya wanalaumiwa kwa kupuuza baadhi ya kesi za dhulma za kijinsia hasa za wanandoa. Shirika la human rights watch limetoa ripoti iitwayo ‘sina pa kuenda’ inayoashiria kwamba,wanawake na wasichana huendelea kuishi na waliowadhulumu katika jamii kwa uoga. Huenda washukiwa walishtakiwa na kesi ikasambaratika kwa kukosa ushahidi au polisi hawakutilia maanani kesi na washukiwa wakasaliwa huru.

Mwanasheria anayendesha kesi za wanawake waliodhulumiwa jijini Nairobi Naomi Kajaira anasema, kesi hukaa mahakamani hata Zaidi ya miaka miwili na kusababisha waathirika kukosa Imani na idara ya mahakama.

Mwathirika Elizabeth anaeleza kwamba,maisha ya kuanza upya baada ya ndoa kuvunjika kutokana na dhulma si rahisi “ Sijui kama nitarudi tena kwa mume wangu,sijapanga chochote”

Lakini Wanachotaka wadau kutoka kwa idara husika za serekali ni usalama wa waathiriwa wa dhulma za kijinsia wanapotafuta usaidizi na haki itelekezwe.