(Video) Masalale! Nguva (Mermaid) adaiwa kuonekana kwenye bahari la Hindi

Muhtasari

‚ÄĘKatika video hiyo, kiumbe mfano wa nguva kinaonekana kikiwa kimelazwa kando ya bahari huku umati wa watu ukiwa umezingira.

Je, unaamini uwepo wa nguva (Mermaid) 

Video inayoonyesha kile ambacho wengi wanadai kuwa nguva imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo, kiumbe mfano wa nguva kinaonekana kikiwa kimelazwa kando ya bahari huku umati wa watu ukiwa umezingira.

Baadhi ya wanamitandao wamedai kwamba kiumbe hicho kilicho na sura nyeusi kilipatikana Bahari la Hindi katika eneo la Ukunda, Kwale.

Hata hivyo, wanamitandao wengine wametilia shaka kiumbe hicho huku wakidai kwamba ni binadamu aliyevalishwa mavazi mfano wa mkia wa nguva.