Jamaa aliyebaka msichana wa miaka 4 kisha kumtoa uhai akamatwa Kirinyaga

Gabriel Muchira Muriithi, 27, alitolewa toka mafichoni yake na kukamatwa na wapelelezi wa jinai siku ya Ijumaa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani ifikapo Jumatatu.

Muhtasari

•Mnamo Agosti 11, mwili wa Ruth Wanjiku Kimani ambaye kufikia kifo chake alikuwa mwanafunzi katika shule ya msingi ya Mugumo ulipatikana kando ya mto Karani, hatua chache kutoka shule yake.

Pingu
Image: Radio Jambo

Polisi katika kaunti ya Kirinyaga wanamzuilia mwanaume mmoja anayeripotiwa kubaka msichana wa darasa la chekechea na kisha kumtoa uhai wiki mbili zilizopita.

Gabriel Muchira Muriithi, 27, alitolewa toka mafichoni yake na kukamatwa na wapelelezi wa jinai siku ya Ijumaa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani ifikapo Jumatatu.

Mnamo Agosti 11, mwili wa Ruth Wanjiku Kimani ambaye kufikia kifo chake alikuwa mwanafunzi katika shule ya msingi ya Mugumo ulipatikana kando ya mto Karani, hatua chache kutoka shule yake.

Upelelezi wa kina kuhusiana na unyama uliotekelezwa dhidi ya msichana huyo ulibainisha kuwa Muchira ndiye mshukiwa mkuu.

Upasuaji wa mwili na uchunguzi wa kidaktari ulidhihirisha kuwa marehemu alikuwa amebakwa kabla ya kuuliwa.