Ripoti: Ukatili na unyanyasaji wa kijinsia bado ni tatizo sugu katika jamii nyingi

Muhtasari

• Ukatili wa kijinsia bado unaendela kudhuru mamilioni ya watu sit u nchini Kenya bali kote ulimwenguni, na limetajwa kuwa mojawapo ya matatizo makubwa ya afya ya umma.

• Ripoti  inapendekeza polisi wanapaswa kuwezeshwa mara kwa mara na ujuzi na nyenzo bora Zaidi za kufuata haki, kuwalenga wahusika wa unyanyasaji na ukatili.

Mhasiriwa wa dhuluma za kijinsia
Image: THE STAR

Ukatili wa kijinsia bado unaendelea kudhuru mamilioni ya watu si tu nchini Kenya bali kote ulimwenguni, na limetajwa kuwa mojawapo ya matatizo makubwa ya afya ya umma.

Unyanyasaji huu wa kijinsia umesalia kuwa donda sugu  katika jamii nyingi ukiwa umejumuisha ukiukwaji wa haki za kibinadamu ambao wengi wanauvumilia kote nchini kwa sababu ya kukosa njia dhabiti za kuripoti visa hivi pindi vinapowasibu.

Viashiria vya ukatili wa kijinsia vinaonesha kuongezeka kwa matukio ya ukatili wa kimwili na kingono pia, yakiwemo matukio ya mauaji ya wapenzi wa kike, ukatili wa kingono, vipigo, visa vya kuvunjika kwa familia, ulazimishwaji wa ndoa za mapema kwa Watoto chini ya umri wa miaka 18, ukeketaji wa wanawake, miongoni mwa maovu mengine.

Ingawa kuna uhaba na ukosefu wa deta za kisasa zinazoonesha kuenea kwa visa hivi vya unyanyasaji nchini Kenya, ni suala la kuvunja moyo sana na la kuogofya kutazama, kusoma na kusikiliza visa hivi vinaporipotiwa kila siku katika mitandao, runinga, majarida na hata kwenye redio.

Naibu wazira kkatika wizara ya jinsia, Racheal Shebesh, wakiwa pamoja na mwakilishi wa kike kaunti ya Nairobi, Esther Passaris wakati wa mkutano wa kitaifa wa dhuluma za kijinsia Oktoba, 2021
Image: KELVIN MUTINDA

Matokeo ya utafiti wa tume ya kitaifa ya jinsia na usawa ya mwaka wa 2016, katika utafiti walioupa mada ya Ukatili wa Kijinsia nchini Kenya, ripoti hiyo ilipendekeza kwamba suala la unyanyasaji wa kijinsia linapaswa kutangazwa janga la kitaifa, miongozo ya sera inapaswa kuimarishwa, uhamasishaji kuundwa na kujumuisha usimamizi wa ukatili wa kijinsia katika mafunzo kwa wahudumu wa afya, wafanyakazi wa shughuli za kijamii, mahakama, vyombo vya usalama na watunga sera wengine kwa ujumla.

Washikadau katika sekta za serikali na zile zisizo za kiserikali wameombwa pia kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuboresha mfumo wa usimamizi wa unyanyasaji wa kijinsia katika ngazi zote kupitia utoaji wa raslimali, kujenga uwezo unaofaa wa wahusika ili kutekeleza ushirikiano jumuishi katika sekta mbalimbali.

Ripoti hiyo pia ilipendekeza polisi kuwezeshwa mara kwa mara na ujuzi na nyenzo bora zaidi za kufuata haki na mbinu mwafaka za kuwatia nguvuni wahusika wa unyanyasaji na ukatili wakijinsia si tu kwa wanawake pekee bali kwa jinsia zote