Babu Owino asema wanafunzi vyuoni wako njaa, hawana hata nguvu ya kula nyama ya binadamu

Aliitaka serikal ikutumia 93M ambazo waliema ndio zilibaki kuwalipa wanafunzi kama HELB

Muhtasari

• 93M zinazodaiwa zilibaki kwenye Hazina ya serikali kuu zipelekwe kwa Wanafunzi/Comrades kama Mkopo(HELB)

BabuOwino ataka serikali kuwapa wanafunzi HELB
BabuOwino ataka serikali kuwapa wanafunzi HELB
Image: facebook

Wikendi iliyopita baadhi ya wanasiasa kutoka mrengo wa Kenya Kwanza waliibua madai kwamab serikali ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta ilifyonza karibu kila kitu kutoka kwa akaunti za serikali.

 Wanasiasa hao wakiongozwa na aliyekuwa seneta maalum Millicent Omanga na seneta wa Nandi Samson Cherargei walisema kwamba uongozi ulioondoka ulibakisha kima cha shilingi milioni 93.7 pekee kwenye hazina ya serikali kuu.

Mbunge wa Embakasi East sasa anaitaka serikali kutumia kiasi hicho cha pesa chote kuwasitiri wanafunzi wa chuo kikuu kupitia mpango wa mikopo ya elimu ya juu, HELB.

Owino ambaye alikuwa kiongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini pamoja pia na kuwa kiongozi wa wanafunzi katika chuo kikuu cha Nairobi kwa muda mrefu anajulikana sana kama mtetezi wa maslahi ya wanafunzi wa vyuo vikuu.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Owino alisema waanfunzi wengi katika vyuo vikuu wako katika njaa kubwana kutaka pesa hizo zilizosemekana kuwa ndio salio pekee la serikal imbele nyuma kutumika kuwasaidia wanafunzi hao.

 Mbunge huyo alisema kwamba wengi wanaishi maisha mabaya vyuoni kutokana na kucheleweshwa kwa pesa hizo za kufadhili masomo na maisha yao wakiwa masomoni.

“93M zinazodaiwa zilibaki kwenye Hazina ya serikali kuu zipelekwe kwa Wanafunzi/Comrades kama Mkopo(HELB). Wenzangu wana njaa kali, hawana nguvu hata ya ‘kula’ nyama ya binadamu,” Babu Owino alisema.