Michelle Ntalami aonesha mazungumzo yake ya mwisho na Edwin Chiloba

"Ubinadamu umepoteza aina ya mtu ambaye alihakikisha wanatumia kila dakika uchao kueneza upendo safi."

Muhtasari

• Ntalami alitamka laana kwa wale waliotekeleza mauaji ya Chiloba na kusema hawatawahi pata amani.

• Ntalami alisimulia jinsi walikutana na Chiloba kwa mara ya kwanza baada ya kuhadithia maisha yake kwa ulimwengu.

Michelle Ntalami amuomboleza Chiloba
Michelle Ntalami amuomboleza Chiloba
Image: Instagram

Mrembo Michelle Ntalami amemuomboleza rafiki yake Edwin Chiloba ambaye aliuawa katika mzozo wa kimapenzi na mpenzi wake mwanaume.

Ntalami alipakia rundo la picha kweney Instagram moja ikiwemo ya mazungumzo baina yao kabla ya kuripotiwa kutoweka na siku kadhaa badae mwili wake kupatikana umesondekwa kwenye sanduku la chuma na kutupwa barabarani.

Chiloba ambaye alikuwa mwanaharakati wa LGBTQ alikuwa rafiki wa Ntalami ambaye pia kwa muda mrefu amekuwa akitajwa kuwa mwanachama wa jamii hiyo inayopigia debe mapenzi ya watu wa jinsia moja.

Kwa wakati mmoja, Ntalami alisemekana kutoka kimapenzi na mwanahabari Makena Njeri lakini mapenzi yao yakagonga mwamba.

Ntalami alisimulia jinsi walivyokutana baada ya kuelezea hadithi ya maisha yake na Chiloba alimfuata faraghani na kufanya mazungumzo naye kuhusu maisha yake ya kimapenzi.

“Tulikutana kupitia MAPENZI yake.♥️ Niliwahi kushiriki hadithi ya kibinafsi na ulimwengu, na ilimgusa sana hivi kwamba alinitafuta ili tu kushiriki baadhi ya upendo na mwanga wake mwenyewe. Ubinadamu umepoteza aina ya mtu ambaye alihakikisha wanatumia kila dakika uchao kueneza upendo safi, usioghoshiwa,” ujumbe mrefu wa Ntalami ulisoma kwa sehemu.

Michelle alisema kuwa ndoto ya Chiloba ilikuwa ni kuwa mwanafasheni mkubwa wa kimataifa la kuahidi kuwa licha ya kufa kwake bado watifanikisha ndoto yake huku pia akitamka laana kuwafuata waliosababisha kifo chake.

“Edwin, ulikuwa na ndoto kubwa ulizoshiriki nami. Tulikuwa tukufikisha hapo.😔 Ndoto za kuwa mwanamitindo duniani kote na kufika kwenye viwanja vya ndege vya Milan na New York. Lakini hawatajua amani kamwe! Wala hawawezi kufifisha mwanga wako. Nakumbuka wakati mmoja wa sanamu zangu, Princess Diana alikufa, na ulimwengu wote ulikuwa katika maombolezo, kwa sababu alijumuisha UPENDO. Sawa na wewe; mtu yeyote anayejumuisha upendo huacha shimo wakati amekwenda,” Ntalami aliomboleza.

Kufikia Jumatatu asubuhi, tayari watu 4 walikuwa wametiwa mbaroni kuhusiana na mauaji ya Chiloba, mshukiwa mkuu akiwa ni Jackton Odhimabo ambaye alikuwa mpenzi wake.