Kitui: Jamaa ajitia kitanzi baada ya kumuua ndugu yake kwa kumkata kata

Jamaa huyo wa miaka 35 walikorofishana na nduguye na akamshambulia kwa panga kabla ya kujinyonga pia.

Muhtasari

• Baada ya kumshambulia ndugu yake kwa panga, alitoroka na kumuacha mahututi.

• Wanakijiji walimkimbiza mwathiriwa hospitalini na kurudi wakapata mtuhumiwa pia amejitia kamba shingoni.

Jamaa amuua ndugu yake kabla ya kujitoa uhai.
Jamaa amuua ndugu yake kabla ya kujitoa uhai.
Image: Screengrab

Tukio la ajabu limeripotiwa kaunti ya Kitui, eneo la Mwingi baada ya mwanamume wa miaka 35 kudaiwa kumuua ndugu yake kwa kumkata kwa upanga kabla ya kujitia kitanzi pia.

Kulingana na ripoti katika runinga ya Citizen, majirani walisema kwamba walisikia kelele na kufka wakapata mwanamume huyo amemvamia ndugu yake kwa panga na kumkatakata kabla ya kutoroka.

Majirani hao waling’an’ana kwa upesi kumhudumia mwathiriwa kwa kumkimbiza hospitalini na waliporudi walianza kumtafuta mtuhumiwa lakini hawakumpata.

Walipochungulia kwa nyumba yake, walimuona yuko ndani na amejitoa uhai.

“Kulikuwa na mzozo katika eneo hilo na wakati tumekimbia kujua mzozo ni wa nini, tulikuta kijana amekatakata ndugu yake na pia ameweza kujiua kabla watu wang’ang’ane na kuvunja mlango wakakuta amefariki kwa kujinyonga,” mkaazi mmoja alisema.

 Wakaazi hao pia walitoa wito kwa vijana haswa ndugu kupata mwafaka wa maelewano wakati tofauto zinapotokea baina yao, huku pia wakionesha mashaka kwamba huenda vijana wengi wameathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zinawaongoza katika vichwa vyao kufanya visa vya ajabu katika jamii.

“Tunaomba vijana kama kuna kitu umekula na inakusumbua kwa kichwa yako, enda kanisani, rudi kwa Mungu uombewe ili vitendo kama hivi visijirudie tena katika macho yetu,” mwingine alitoa himizo.