Bei ya petroli yapanda huku dizeli ikipungua

Muhtasari

• Bei hizi mpya zinajumuisha ushuru wa VAT wa asilimia 8 kuambatana na sheria ya kifedha ya mwaka 2018.

• Bei ya mafuta taa haijabadilika.

• Bei hizi mpya zinaanza kutekelezwa leo Jumatano saa sita usiku.

Bei ya mafuta ya petroli imepanda kwa senti 72 kwa lita huku ile ya dizeli ikipungua kwa shilingi 2.18 kwa lita kulingana na bei zilizotangazwa na mamlaka ya kudhibiti kawi nchini EPRA siku ya Jumatano.

Bei ya mafuta taa haijabadilika. Bei hizi mpya zinaanza kutekelezwa leo Jumatano saa sita usiku.

Bei hizi mpya zinajumuisha ushuru wa VAT wa asilimia 8 kuambatana na sheria ya kifedha ya mwaka 2018.

 

Kulingana na mamlaka hiyo petroli sasa itauzwa shilingi 104.86 kwa lita Mombasa, dizeli 90.53 huku mafuta taa yakiuzwa shilingi 81.37.

Katika eneo la Nairobi na vyungani mwake, petroli itauzwa shilingi 107.27 huku dizeli ikiuzwa shilingi 92.91 nayo mafuta taa yakiuzwa shilingi 83.73.

Wakaazi wa Nakuru watanunua lita moja ya petroli kwa shilingi 106.96, dizeli 92.85 na mafuta taa 83.69.

Wenye magari Kisumu watanunua petroli kwa shilingi 107.88, dizeli itawagharimu 93.77 nayo mafuta taa yakiuzwa shilingi 84.60 kwa lita.